Jinsi ya kuagiza ukitumia kikapu
Unapotembelea katalogi ya biashara kwenye WhatsApp, unaweza kutumia kitufe cha Tumia Biashara Ujumbe kuanzisha mazungumzo au utumie kitufe cha Ongeza kwenye Kikapu ikiwa upo tayari kuagiza bidhaa unayoiangalia.
Kuweka bidhaa kwenye kikapu
- Fungua WhatsApp.
- Fungua soga yako au jalada la biashara ambako ungependa kuagiza bidhaa.
- Gusa aikoni ya kitufe cha ununuzi
iliyoorodheshwa kando ya jina la biashara ili ufikie katalogi yake. - Baada ya katalogi kufunguka, kagua bidhaa ambazo ungependa kuagiza.
- Gusa bidhaa unayopenda.
- Gusa Ongeza kwenye Kikapu katika bidhaa ambazo ungependa kuagiza.
- Au, unaweza pia kugusa Tumia Biashara Ujumbe ikiwa ungependa kutumia biashara ujumbe kuhusu bidhaa.
Kubadilisha bidhaa zilizo kwenye kikapu chako
- Gusa aikoni ya kikapu ili uone bidhaa zote ulizoweka kwenye kikapu chako.
- Gusa Ongeza zaidi ikiwa ungependa kurudi kwenye katalogi ili uendelee kuongeza bidhaa zaidi.
- Pia unaweza kubadilisha idadi ya kila bidhaa uliyoweka kwenye kikapu chako.
Kuagiza
- Baada ya kusasisha kikapu chako, gusa aikoni ya tuma ili umtumie muuzaji kikapu chako kama ujumbe wa WhatsApp.
- Baada ya kutuma, utaona maelezo ya agizo lako kwa kugusa kitufe cha Angalia kikapu katika dirisha la soga na muuzaji.
Ikiwa ungependa kuuliza kuhusu bidhaa nyingi zilizoorodheshwa katika katalogi ya muuzaji, unaweza kuziongeza zote kwenye kikapu na kutuma maswali yako katika ujumbe mmoja. Agizo halijakamilika hadi lithibitishwe na muuzaji.
Pakua mchoro huu wenye maelezo kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuongeza bidhaa kwenye kikapu chako.