Jinsi ya kuongeza hifadhi kwenye WhatsApp
Unaweza kuangalia ni kiasi gani cha nafasi kinachukuliwa na WhatsApp kwenye kifaa chako na kuongeza nafasi kwa kufuta vipengee.
Tazama hifadhi
- Nenda kwa WhatsApp Mipangilio.
- Gusa Hifadhi na Data > Dhibiti Hifadhi.
Kiasi cha nafasi kinachotumiwa kwenye kifaa chako na Midia ya WhatsApp na Programu na Vipengee Vingine vinaonyeshwa juu ya skrini.
Kagua na futa vipengee
Unaweza kuongeza nafasi kwa kufuta vipengee ambavyo ni vikubwa au vimesambazwa mara nyingi. Unaweza pia kufuta vipengee kwa kila soga.
Kukagua vipengee
- Nenda kwa WhatsApp Mipangilio.
- Gusa Hifadhi na Data > Dhibiti Hifadhi.
- Gusa Kubwa kuliko MB 5, Imesambazwa Mara Nyingi, au chagua soga maalumu.
- Unaweza kugusa aikoni ya kupanga ili upange kwa Mpya kabisa, Nzee zaidi, au Kubwa zaidi.
- Ukubwa wa faili wa vipengee unaonyeshwa kwenye kona ya juu ya kipengee.
- Gusa kipengee ili kukikagua.
Kufuta vipengee
Ukichagua kufuta kipengee, kitafutwa kutoka kwa midia yako ya WhatsApp. Vipengee vilivyofutwa bado vinaweza kuhifadhiwa kwenye kifaa chako. Kama una nakala kadhaa za kipengee, utahitajika pia kufuta nakala zote ili kuongeza nafasi.
- Nenda kwa WhatsApp Mipangilio.
- Gusa Hifadhi na Data > Dhibiti Hifadhi.
- Gusa Kubwa kuliko MB 5, Imesambazwa Mara Nyingi, au chagua soga maalumu.
- Unaweza:
- Kuchagua vipengee vyote: Gusa Chagua Vyote kama unataka kufuta vipengee vyote kwa mara moja.
- Futa vipengee binafsi: Gusa kipengee unachotaka kukifuta. Chagua vipengee vingine vya kufuta kwa mara moja
- Gusa Futa
- Kama ulichagua vipengee vyenye nyota, unaweza kuchagua Kufuta Vyote Isipokuwa Vyenye Nyota au Futa Vyote.
- Gusa Futa Kipengee au Futa Vipengee.
- Kama ukichagua vipengee kadhaa, gusa Futa Kipengee na Nakala Yoyote au Futa Vipengee na Nakala Zozote.
Kufuta vipengee kwa kuvitafuta
Unaweza pia kufuta kipengee binafsi kwa kutumia kipengele cha kutafuta.
- Kwenye Soga gusa, telezesha chini kuonyesha kitufe cha Tafuta.
- Gusa Picha, Video, au Nyaraka.
- Gusa kipengee unachotaka kufuta.
- Gusa Futa
> Futa Kwangu.
Arifa za nafasi ndogo ya hifadhi
Ikiwa kiasi cha nafasi iliyopo kwenye kifaa chako kinafikia kiasi cha chini sana, WhatsApp huenda isiweze kufanya kazi vizuri. Kama hili likitokea, WhatsApp inaweza kukuuliza uongeze nafasi ili uendelee kutumia programu hii.
Unaweza pia kuongeza nafasi kwa kufuta programu usizotumia au video kubwa, picha au faili zilizohifadhiwa kwenye simu yako. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuongeza nafasi ya hifadhi kwenye simu yako nje ya WhatsApp, tafadhali tembelea tovuti ya Msaada ya Apple.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kuongeza nafasi kwenye WhatsApp kwenye Android
- Kuhusu kikomo cha kusambaza