Unaweza kuifuta akaunti yako ukiwa kwenye WhatsApp. Kufuta akaunti yako ni mchakato usioweza kutenduliwa, ambao hatuwezi kuubatilisha hata kama umeufanya kimakosa.
Kufuta akaunti yako
- Fungua WhatsApp.
- Nenda kwenye Mipangilio > Akaunti > Futa Akaunti Yangu.
- Weka nambari yako ya simu katika mfumo kamili wa kimataifa kisha uguse Futa Akaunti Yangu.
Kufuta akaunti yako kutafanya yafuatayo:
- Kutafuta taarifa na picha ya jalada ya akaunti yako.
- Kutakufuta kutoka kwenye vikundi vyote vya WhatsApp.
- Kutafuta chelezo ya historia ya ujumbe wako wa WhatsApp.
Ukiifuta akaunti yako:
- Huwezi kurejesha upatikanaji wa akaunti yako.
- Inaweza kuchukua hadi siku 90 kutoka mwanzo wa mchakato wa kufuta ili kufuta taarifa zako zilizo kwenye WhatsApp. Nakala ya taarifa zako huenda pia zikabaki baada ya siku 90 kwenye hifadhi ya chelezo ambayo huwa tunaitumia ili kurejesha taarifa endapo kuna mkasa, hitilafu ya programu au tukio jingine la kupoteza data. Hutapata taarifa zako kwenye WhatsApp katika kipindi hicho.
- Hutaathiri taarifa zako zinazohusiana na vikundi ulivyounda au taarifa kukuhusu ambazo watumiaji wengine wanazo, kama vile nakala ya ujumbe uliowatumia.
- Nakala za nyenzo kama vile rekodi za kumbukumbu zinaweza kubaki katika hifadhidata yetu lakini hazitahusishwa na taarifa binafsi zinazoweza kukutambulisha.
- Tunaweza pia kuhifadhi taarifa zako kwa ajili ya mambo kama vile, masuala yanayohusu sheria, ukiukaji wa masharti, au juhudi za kuzuia madhara.
- Tafadhali rejea sehemu ya Sheria na Ulinzi katika Sera yetu ya Faragha kwa maelezo zaidi.
- Taarifa yako uliyoshiriki na Mashirika ya Facebook pia itafutwa.
Rasilimali zinazohusiana:
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufuta akaunti yako kwenye: Android | KaiOS