Kuhusu vipengele vya ufikivu kwenye WhatsApp
Unaweza kuwezesha vipengele vya ufikivu kwenye WhatsApp kupitia mipangilio ya simu yako. Kwenye iPhone, unaweza:
- Kutumia VoiceOver ikiwa ungependa kuwasiliana na kifaa chako ukitumia majibu yanayotamkwa na ishara za VoiceOver. Unaweza kutumia VoiceOver ili ikusaidie kukuongoza unapojipiga picha ukitumia kamera ya WhatsApp.
- Kutumia Siri kutuma au kusoma ujumbe na kupiga simu kwenye WhatsApp.
- Kurekebisha mwonekano au ukubwa wa maandishi, kukuza au kuvuta karibu skrini yako na kurekebisha utofautishaji au rangi.
Kwa maelezo na maagizo zaidi kuhusu vipengele vya ufikivu vinavyopatikana kwenye simu yako, tafadhali tembelea tovuti ya Msaada ya Apple.
Ili uripoti matatizo yanayohusiana na ufikivu au ushiriki mapendekezo, unaweza kuwasiliana nasi kupitia accessibility@support.whatsapp.com.