Njia ya rahisi ya kuhamisha data ya WhatsApp kwa simu mpya ni kwa kutumia Google Drive. Tunapendekeza kuunganisha simu yako na Wi-Fi kabla ya kucheleza soga zako kupitia Google Drive, kwa sababu faili za chelezo zinaweza kutofautiana kwa ukubwa na hutumia data ya rununu, kusababisha gharama ziada.
Mahitaji
Ili kutumia chelezo ya Google Drive, unahitaji kuwa na:
Akaunti ya Google imewezeshwa kwenye simu yako.
Huduma za Google Play zimesakinishwa kwenye simu yako.
Nafasi huru ya kutosha kwenye simu yako kuunda chelezo.
Muunganisho wa intaneti iliyo na nguvu na ni imara.
Kumbuka:
Chelezo za WhatsApp hazihesabiwi tena kwenye kiwango cha hifadhi ya Google Drive.
Chelezo za WhatsApp zinaunganishwa na namba ya simu na akaunti ya Google ambapo ziliundwa.
Chelezo za WhatsApp ambazo hazijasasishwa kwa zaidi ya mwaka mmoja zinaondolewa kiotomatiki kutoka hifadhi ya Google Drive. Ili kuepuka kupoteza chelezo zozote, tunapendekeza kucheleza data yako ya WhatsApp.
Chelezo ya kwanza inaweza kuchukua muda kukamilika. Tafadhali acha simu yako iungane na chanzo cha umeme.
Kila wakati unatengeneza chelezo ya Google Drive kwa kutumia akaunti sawa ya Google, chelezo ya awali itabadilishwa. Hakuna njia ya kurejesha chelezo ya Google Drive ya zamani.
Media na jumbe unazocheleza hazilindwi na ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho wa WhatsApp zikiwepo kwenye Google Drive.
Jinsi ya kuunda chelezo ya Google Drive
Fungua WhatsApp.
Gusa Hiari zaidi > Mipangilio > Soga > Chelezo ya soga.
Gusa Cheleza kwa Google Drive na chagua marudio ya kucheleza isipokua Kamwe.
Chagua akaunti ya Google utakayo tumia kucheleza historia ya soga. Ikiwa hauna akaunti ya Google iliyounganishwa, gusa Ongeza akaunti unapoulizwa kuingiza vitambulishi vyako vya kuingia.
Gusa Cheleza kwa kuchagua mtandao unaotaka kutumia kwa kucheleza. Tafadhali zingatia kwamba kucheleza kwa mtandao wa data ya selula kunaweza kuwa na gharama ziada za data.
Cheleza kwa Google Drive
Unaweza pia kucheleza soga zako kwenye Google Drive wakati wowote.
Fungua WhatsApp.
Gusa Hiari zaidi > Mipangilio > Soga > Chelezo ya soga.
Gusa CHELEZA.
Kusanidi mipangilio yako ya chelezo ya Google Drive
Badili marudio ya chelezo ya Google Drive
Fungua WhatsApp.
Gusa Hiari zaidi > Mipangilio > Soga > Chelezo ya soga.
Gusa Cheleza kwa Google Drive.
Chagua marudio ya chelezo.
Badili akaunti unayotaka kutumia kwa chelezo
Fungua WhatsApp.
Gusa Hiari zaidi > Mipangilio > Soga > Chelezo ya soga.
Gusa Akaunti na chagua akaunti ambayo unataka kuchelezea historia ya soga zako.
Kumbuka: ukibadili akaunti yako ya Google, hutaweza kupata chelezo zako ambazo zinaunganishwa na akaunti tofauti ya Google.
Badili mtandao unayotaka kutumia kwa chelezo
Fungua WhatsApp.
Gusa Hiari zaidi > Mipangilio > Soga > Chelezo ya soga.
Gusa Cheleza kwa na chagua mtandao ungependa kutumia kucheleza.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kurejesha historia ya soga yako kwenye Android.