WhatsApp inapatikana kwa zaidi ya lugha 40 na mpaka 60 kwenye Android. Kwa sheria ya jumla, WhatsApp hufuata lugha ya simu yako. Kwa mfano, ukibadilisha lugha ya simu yako kwa Kihispania, WhatsApp itakuwa kwa Kihispania kiotomatiki.
Kubadilisha lugha ya simu yako:
- Android: Nenda kwenye simu yako Mipangilio > Mfumo > Lugha & pembejeo > Lugha. Gusa na shikilia lugha kuiweka juu, au gusa Ongeza lugha
.
- iPhone: Nenda Mipangilio ya iPhone
> Jumla > Lugha & Eneo > Lugha ya iPhone. Chagua lugha, halafu gusa Imekamilika > Badili {lugha}.
- Windows Phone: Nenda kwenye simu yako Mipangilio > Saa & lugha > Lugha. Gusa Ongeza lugha, au gusa na shikilia lugha > kisha gusa Sogeza juu mpaka ifike sehemu ya juu. Tafadhali kumbuka utahitaji kuanzisha upya simu yako kwa mabadiliko haya kutimizwa.
- KaiOS: Bonyeza Mipangilio kwenye menyu ya programu > sogeza kwa upande kuchagua Utambulisho > sogeza chini na bonyeza Lugha > bonyeza Lugha > chagua lugha unayotaka kutumia > bonyeza SAWA au CHAGUA.
Hiari zaidi inapatikana kwa nchi zinazowezeshwa
Ikiwa unatumia simu ya Android. unaweza kuwa na hiari ya kubadili lugha ya WhatsApp kutoka ndani ya programu. Kufanya hivyo:
- Fungua WhatsApp.
- Gusa Hiari zaidi
> Mipangilio > Soga
> Lugha ya programu.
- Katika popup inayoonekana, chagua lugha unayotaka.
Kumbuka: Ikiwa huoni hiari hii, labda haiwezeshwi katika nchi yako.