Kipengele cha Badili Namba kinakuwezesha kubadili namba ya simu yako inayohusiana na akaunti yako ya WhatsApp kwenye simu hiyohiyo. Kipengele hiki kina lengo la kutumiwa kabla ya kuthibitisha namba mpya.
Ikiwa una namba ya simu mpya na simu mpya, tafadhali soma nakala hii.
Kwa kutumia kipengele cha Badili Namba kwenye WhatsApp utafanya yafuatayo:
- Hamisha maelezo ya akaunti yako (pamoja na maelezo ya jalada), vikundi na mipangilio kutoka kwenye namba ya simu ya zamani kuweka kwenye namba mpya ya simu, na
- Futa akaunti inayohusiana na namba ya simu ya zamani, ili waasiliani wako wasione tena namba ya simu ya zamani kwenye orodha zao za waasiliani wa WhatsApp.
Ukitumia kipengele cha Badili Namba, historia ya soga itaendelea kupatikana kwenye simu yako iliyo na namba mpya ya simu kama tu utaendelea kutumia simu hiyo.
Kabla ya kuanza mchakato wa Badili Namba
- Hakikisha kuwa namba mpya ya simu inaweza kupokea SMS na/au simu ina muunganisho wa data ulio hai.
- Hakikisha kuwa namba ya simu ya zamani sasa imehakikishwa kwenye Whatsapp ya simu yako. Unaweza kuona kuwa namba imethibitishwa kwenye WhatsApp kwa kupitia WhatsApp > Menyu
> mipangilio > jalada.
Kumbuka: Unapobadilisha namba yako ya WhatsApp phone number, waasiliani wako hawatajulishwa kibinafsi kuhusu ubadiliko. Washiriki wanaoshiriki katika soga za kikundi na wewe tu ndiyo wataona kuwa umebadilisha namba. Kwa uzoefu wa ujumbe usio na shida, wajulishe waasiliani wako ya kuwa namba yako itabadilika kabla ya kuanza mchakato huu.
Kubadilisha namba yako ya simu
Kubadili namba yako ya simu ndani ya WhatsApp, fuata hatua hizi:
- Ingiza kadi mpya ya SIM ilio na namba mpya kwenye simu yako.
- Fungua WhatsApp.
- Angalia kama nambari ya simu ya zamani imethibitishwa. Unaweza kuona kuwa namba imethibitishwa kwenye WhatsApp kwa kupitia WhatsApp > Menyu
> mipangilio > jalada.
- Gusa Menyu
> mipangilio > akaunti > badili namba yangu > endelea.
- Ingiza namba ya simu ya zamani kwenye sanduku la juu.
- Ingiza namba ya simu mpya kwenye sanduku la juu.

- Gusa mbele.
- Ukiwasha waarifu waasiliani, unaweza kuchagua kama unataka kuwaarifu waasiliani wote, waasiliani ambao nina soga nao au kibinafsi.
- UkichaguaKibinafsi, utahitaji kutafuta na kuchagua waasiliani unaotaka kuwaarifu > gusa alama ya sahihi au imekamilika.
- Gusa kubali iliyopo upande wa chini kwenye skrini kuendelea.
- Utaulizwa kuthibitisha namba yako ya simu mpya.
Jifunze jinsi ya kubadili namba kwenye: Android | iPhone