WhatsApp haina haja ya kuchukua picha zako. Tunataka tu kurahisisha uwezo wa wewe kuwa na ubora wa mazungumzo ya kipicha na wale walio karibu nawe. Faragha na usalama wako ni muhimu kwetu, na tunataka ujisikie kuwa unaweza kutumia programu tumishi kwa uhuru.
WhatsApp ina kitufe cha picha ambacho kinakuruhusu kuchukua picha na video kwa kutumia kamera ya simu yako moja kwa moja. Kuweza kutumia kipengele hiki, unahitaji kuruhusu WhatsApp kufungua kamera yako unapoulizwa. Unahakikishiwa kuwa, WhatsApp kamwe haitachukua picha au video kwa niaba yako.