Ikiwa ungependa kuwasiliana na wateja wako kwenye WhatsApp ukitumia API yetu ya Business, tunakuhimiza ufanye kazi na Watoaji wa Suluhisho ya Kibiashara (BSP) walio katika orodha yetu. Hii ni jumuiya ya watoaji suluhisho ambao wana weledi katika API ya WhatsApp Business. BSP hizi zinaweza kukusaidia kuzungumza na wateja wako kwenye WhatsApp kwa ajili ya matumizi yanayoruhusiwa ya msaada kwa mteja na arifa za kibinafsi kwa muda mzuri.
Kama ilivyoelezwa kwenye waraka wetu rasmi, wahusika wengine wanaotoa huduma zisizoidhinishwa kwenye jukwaa letu, kama vile ujumbe wa kiotomatiki au zinazotumwa kwa wingi, wanafanya hivyo kwa kukiuka Masharti yetu ya Huduma. Ikiwa umekuwa ukifanya kazi na mtu mhusika mwingine kutoa huduma isiyoidhinishwa, huenda hutaweza kutuma ujumbe nao kwenye WhatsApp. Tunapendekeza ufanye kazi na BSP zetu zilizoidhinishwa badala yake.
Kumbuka: Orodha iliyoshirikiwa ya BSP ni kwa ajili ya marejeo tu. Tunapendekeza ufanye uangalifu wako mwenyewe wa kampuni unayochagua kufanya kazi nayo.