Kufanya kazi na Watoaji wa Suluhisho
Jukwaa la WhatsApp Business huenda bado halipatikani kwako. Kagua maktaba yetu ya maudhui ya msaada wa Jukwaa la WhatsApp Business hapa.
Ikiwa ungependa kuwasiliana na wateja wako kwenye WhatsApp ukitumia Jukwaa la WhatsApp Business, tunakuhimiza ufanye kazi na Watoaji wa Suluhisho za Biashara (BSP) walio katika orodha yetu ya WhatsApp Business. Hii ni jumuiya ya watoaji suluhisho ambao wana weledi katika Jukwaa la WhatsApp Business. Mashirika haya yanaweza kukusaidia kuwasiliana na wateja wako kwenye WhatsApp kwa matumizi yanayoruhusiwa ya msaada kwa wateja na kutoa taarifa za binafsi katika muda unaofaa.
Kama ilivyoelezwa kwenye waraka wetu rasmi, wahusika wengine wanaotoa huduma zisizoidhinishwa kwenye jukwaa letu, kama vile ujumbe wa kiotomatiki au unaotumwa kwa wingi, wanafanya hivyo kwa kukiuka Masharti yetu ya Huduma. Ikiwa umekuwa ukifanya kazi na mhusika mwingine kutoa huduma isiyoidhinishwa, huenda hutaweza kutuma ujumbe kupitia huduma yao kwenye WhatsApp. Tunapendekeza ufanye kazi na watoa huduma tuliowaidhinisha.
Kumbuka: Orodha iliyoshirikiwa ya BSP ni kwa ajili ya marejeo tu. Tunapendekeza ufanye uchunguzi wako mwenyewe kuhusu kampuni unayochagua kufanya kazi nayo.