Kama ilivyotangazwa kwenye blogi yetu, WhatsApp inachunguza njia za kukuunganisha na biashara zilizo muhimu kwako. Programu ya WhatsApp Business husaidia biashara ndogo kuanzisha uwepo rasmi na hufanya iwe rahisi kujibu wateja.
Tunaunda pia zana mpya kwa kampuni zinazofanya kazi kwa kiwango kikubwa, kama vile ndege, tovuti za biashara za mtandaoni na benki. Biashara hizi zitaweza kutumia suluhisho letu la WhatsApp Business kuwapa wateja habari zakusaidia kama mda wa ndege, uthibitisho wa utoaji na sasisho zingine, na pia kutoa msaada kwa wateja.
Ukitaka kusimamisha biashara kuwasiliana na wewe, unaweza kuwazuia. Jifunze jinsi ya kuzuia au kuruhusu waasiliani kwenye: Android | iPhone