Mara kwa mara, biashara inaweza kutumia mtoaji wa suluhisho ili kusaidia kupata zana zinazohitaji kutuma na kupokea ujumbe kutoka kwako. Watoaji hawa wa suluhisho wanaweza kutoa huduma kama vile kusoma, kuhifadhi na kujibu ujumbe kwa niaba ya biashara.
Baadhi ya biashara na watoaji wa huduma1 hutumia kampuni kuu ya WhatsApp, ambayo ni Facebook, ili ihifadhi na kuwajibu wateja. Ingawa Facebook haitatumia ujumbe wako moja kwa moja kubaini matangazo utakayoona, biashara zitaweza kutumia soga zinazopokea kwa madhumuni yao ya kimauzo, ambayo huenda yakajumuisha kutangaza kwenye Facebook. Unaweza kuwasiliana na biashara husika wakati wowote ili upate maelezo zaidi kuhusu desturi zao za faragha.
1 Mwaka wa 2021.