Kufikia Jukwaa la WhatsApp Business
Jukwaa la WhatsApp Business huenda bado halipatikani kwako. Kagua maktaba yetu ya maudhui ya msaada wa Jukwaa la WhatsApp Business hapa.
Ili kuwasiliana na wateja kwenye Jukwaa la WhatsApp Business, fungua Akaunti ya WhatsApp Business.
Ikiwa unatengeneza kwa ajili ya kampuni yako, unda akaunti kupitia Hati ya Wasanidi wa WhatsApp.
Ikiwa wewe ni Mtoa Huduma za Biashara (BSP), unaweza kuunda akaunti kwenye Akaunti ya Biashara ya Meta.
Ikiwa unafanya kazi na BSP ili kuunganisha mifumo na WhatsApp, unaweza kuunda akaunti kupitia mtiririko uliojumuishwa wa kujisajili.