Akaunti yako ya WhatsApp inaweza tu kuthibitishwa na namba moja kwa kifaa kimoja. Ukiwa na SIM mbili kwenye simu moja, tafadhali zingatia kwamba bado ni lazima uchague namba moja kuthibitisha kwa WhatsApp. Hakuna hiari ya kuwa na akaunti moja ya WhatsApp na namba mbili za simu.
Kama Ukijaribu kubadilisha mara kwa mara akaunti yako ya WhatsApp kati ya vifaa tofauti, kwa wakati fulani, unaweza kuzuiliwa kuthibitisha tena akaunti yako. Tafadhali usirudierudie kubadilisha mara kwa mara vifaa na namba tofauti.