Jinsi ya kudhibiti mipangilio ya uhakiki wa hatua mbili
Unaweza kudhibiti mipangilio ya uhakiki wa hatua mbili kwenye akaunti yako ya WhatsApp. Una hiari ya kuwezesha au kulemaza kipengele hiki, kubadilisha PIN au kusasisha anwani ya barua pepe inayohusishwa na uhakiki wa hatua mbili.
Wezesha uhakiki wa hatua mbili
- Fungua WhatsApp Mipangilio.
- Gusa Akaunti > Uhakiki wa hatua mbili > Wezesha.
- Chagua na ingiza PIN ya tarakimu sita na ithibitishe.
- Toa anwani ya barua pepe unayoweza kuifikia au gusa Ruka kama huhitaji kuongeza anwani ya barua pepe. Tunapendekeza kuongeza anwani ya barua pepe kwa kukuwa kinakuruhusu kuweka upya uhakiki wa hatua mbili na kusaidia kulinda akaunti yako.
- Gusa Ifuatayo.
- Thibitisha anwani ya barua pepe na gusa Hifadhi au Imekamilika.
Kama hutaongeza anwani ya barua pepe na ukisahau PIN yako, utahitaji kusubiri siku 7 kabla ya kuweka upya PIN yako. Kwa kuwa hatuthibitishi hii anwani ya barua pepe ili kuthibitisha uhakika wake, hakikisha kuwa unatoa anwani ya barua pepe sahihi unayoweza kuifikia.
Lemaza uhakiki wa hatua mbili:
- Fungua WhatsApp Mipangilio.
- Gusa Akaunti > Uhakiki wa hatua mbili >Lemaza > Lemaza.
Badilisha PIN yako ya uhakiki wa hatua mbili
- Fungua WhatsApp Mipangilio.
- Gusa Akaunti > Uhakiki wa hatua mbili > Badilisha PIN.
Ongeza anwani ya barua pepe
- Fungua WhatsApp Mipangilio.
- Gusa Akaunti > Uhakiki wa hatua-mbili > gusa Ongeza Anwani ya Barua pepe.
Badilisha anwani ya barua pepe
- Fungua WhatsApp Mipangilio.
- Gusa Akaunti > Uhakiki wa hatua mbili > gusa Badilisha Anwani ya Barua pepe.
Rasilimali zinazohusiana:
Kuhusu uhakiki wa hatua mbili