Uhakiki wa hatua mbili ni kipengele cha hiari kinachoongeza usalama zaidi kwenye akaunti yako ya WhatsApp. Utaona skrini ya uhakiki wa hatua mbili baada ya kusajili nambari yako ya simu kwa ufanisi kwenye WhatsApp. Unaweza kujifunza jinsi ya kuwezesha uhakiki wa hatua mbili kwenye makala haya.
Unapowezesha uhakiki wa hatua mbili, una hiari ya kuingiza anwani yako ya barua pepe. Hii ina ruhusu WhatsApp kukutumia barua pepe yenye kiungo cha kuweka upya PIN yako kama ukiisahau na pia inakusaidia kulinda akaunti yako.
Ili kukusaidia kukumbuka PIN yako, WhatsApp itakuuliza mara kwa mara uingize PIN yako. Kwa bahati mbaya, hakuna hiari ya kulemaza hii bila kulemaza kipengele cha uhakiki wa hatua mbili. Jifunze zaidi kuhusu kusimamia mipangilio ya uhakiki wa hatua mbili kwenye makala haya.
Dokezo: PIN ya uhakiki wa hatua mbili ni tofauti na msimbo wa usajili wa tarakimu 6 unaoupokea kupitia kwa SMS au simu. Unaweza jifunze zaidi kuhusu usajili kwenye makala haya.
Jifunze jinsi ya kulinda akaunti yako.