Sababu ya kawaida kwa nini huwezi kutuma au kupokea ujumbe wa WhatsApp ni muunganisho dhaifu wa intaneti. Jifunze jinsi ya kutatua matatizo ya muunganisho kwenye: Android | iPhone
Ikiwa una hakika kuwa simu yako imeunganishwa kwenye intaneti, kuna sababu chache zinazofanya jumbe za WhatsApp zisipite:
Simu yako inahitaji kuanzishwa tena au kuzima na kuwashwa.
Mwasiliani unayewasiliana naye amezuia namba yako. Pata maelezo zaidi kwenye makala hii.
Haujamaliza mchakato wa uthibitisho wa awali. Jifunze kuhusu kuthibitisha kwenye: Android | iPhone.
Namba ya mwasiliani ambaye unajaribu kumtumia ujumbe kwenye WhatsApp haijahifadhiwa kwa usahihi kwenye simu yako. Jifunze muundo sahihi wa kila namba ya simu hapa.