Jinsi ya kushirikisha hadhi yako ya WhatsApp kwenye programu zingine
Kwenye Android na iPhone, una hiari ya kushirikisha sasisho za hadhi zako za WhatsApp kwenye Hadithi za Facebook na programu zingine. Jifunze zaidi kuhusu faragha ya hadhi kwenye makala hii.
Kushirikisha sasisho ya hadhi yako kwenye Hadithi za Facebook
Una hiari mbili za kushirikisha kulingana na kama unataka kushirikisha sasisho ya hadhi mpya au ya zamani:
Shirikisha sasisho ya hadhi mpya: Chini ya Hadhi yangu, gusa Shirikisha kwenye Hadithi ya Facebook. Ukiulizwa, gusa Ruhusu au Fungua kufungua programu ya Facebook. Kwenye programu ya Facebook, chagua watu unaotaka kushirikishia, kisha gusa Shirikisha Sasa. Tafadhali kumbuka kuwa hiari ya Shirikisha kwenye Hadithi ya Facebook itapotea mara unapoenda kwenye tab nyingine.
Shirikisha sasisho ya hadhi ya zamani: Gusa Hadhi yangu kwenye iPhone au Zaidi kwa Hadhi yangu kwenye Android. Kisha, gusa Zaidi ( au ) karibu na sasisho ya hadhi unayotaka kushirikisha, kisha gusa Shirikisha kwenye Facebook. Ukiulizwa, gusa Ruhusu au Fungua kufungua programu ya Facebook. Kwenye programu ya Facebook, chagua watu unaotaka kushirikishia, kisha gusa Shirikisha Sasa.
Baada ya kushirikisha sasisho ya hadhi, WhatsApp itafunguka tena.
Kumbuka:
Ikiwa una sasisho nyingi za hadhi, unaweza kuchagua zile ambazo unataka kushirikisha kwenye Hadithi za Facebook.
Kipengele hiki kinapatikana tu kama ume sakinisha mojawapo za programu zifuatazo kwenye kifaa chako: Facebook kwenye Android, Facebook Lite kwenye Android au Facebook kwenye iOS.
Kushirikisha sasisho ya hadhi yako kwenye programu zingine
Una hiari mbili za kushirikisha kulingana na kama unataka kushirikisha sasisho ya hadhi mpya au ya zamani:
Shirikisha sasisho ya hadhi mpya: Chini ya Hadhi yangu, gusa Shirikisha ( au ). Tafadhali kumbuka kuwa hiari ya Shirikisha itapotea mara unapoenda kwenye tab nyingine.
Shirikisha sasisho ya hadhi ya zamani: Gusa Hadhi yangu kwenye iPhone au Zaidi kwa Hadhi yangu kwenye Android. Kisha, gusa Zaidi ( au ) karibu na sasisho ya hadhi unayotaka kushirikisha, kisha gusa Shirikisha.
Kwenye trei ya kushirikisha inayotokea, gusa programu unayotaka kushirikishia sasisho ya hadhi yako.