Sasisho zako za hali zinaweza tu kuonwa na mtu ikiwa una nambari yake ya simu kwenye kitabu chako cha anwani na ana nambari yako ya simu kwenye kitabu chake cha anwani. Unaweza kuchagua kushirikisha sasisho za hali zako na waasiliani wako wote, au kwa waasiliani unaowachagua tu. Kimsingi, sasisho za hali zako zinashirikishwa kwa waasiliani wako wote.
Waasiliani wangu: Waasiliani wote wataona sasisho za hali zako.
Waasiliani wangu isipokua...: Waasiliani wako wote isipokua watu unaowachagua wataona sasisho zako za hali.
Shirikisha tu na...: Waasiliani wako tu unaowachagua ndio wataona sasisho zako za hali.
Dokezo:
Mabadiliko kwenye mipangilio yako ya faragha hayataathiri sasisho za hali ambazo tayari umetuma.
Kama umelemaza taarifa za kusomwa, hutaweza kuona ni nani aliyeona sasisho za hali yako. Kama mwasiliani amelemaza taarifa za kusomwa, hutaweza kuona kama ameona sasisho za hali yako.
Kushirikisha sasisho za hali kwenye Hadithi za Facebook na programu zingine
Ukishiriki sasisho lako la hali, maudhui ya sasisho la hali yako yatashirikishwa na programu zingine. Unaposhiriki sasisho lako la hali, WhatsApp haitashirikisha taarifa za akaunti yako na Facebook au programu zingine.
Rasilimali zinazohusiana
Fahamu jinsi ya kutumia hali kwenye: Android | iPhone
Fahamu jinsi ya kushiriki sasisho za hali ya WhatsApp katika programu nyingine kwenye makala haya.