Ili kukupa muda wa kutosha kuhakiki mabadiliko kwa kasi na muda wako mwenyewe, tumeongeza muda wa kuanza kutumika hadi tarehe 15 Mei. Ikiwa utakuwa hujakubali kufikia wakati huo, WhatsApp haitafuta akaunti yako. Hata hivyo, hutakuwa na utendaji kamili wa WhatsApp hadi ukubali. Kwa muda mfupi, utaweza kupokea simu na arifa, lakini hutaweza kusoma na kutuma ujumbe kwenye programu.
Una hiari zifuatazo:
- Bado unaweza kukubali masasisho baada ya tarehe 15 Mei.
- Kabla ya tarehe 15 Mei, unaweza kupakua historia yako ya soga kwenye Android au iPhone na upakue ripoti ya akaunti yako. Ikiwa ungependa kufuta akaunti yako kwenye Android, iPhone, au KaiOS, tunapendekeza usichukue uamuzi huo. Ni hatua ambayo haiwezi kutenduliwa kwa vile hufuta historia yako ya ujumbe, hukuondoa kwenye vikundi vyako vyote vya WhatsApp na kufuta chelezo zako za WhatsApp.
- Ikiwa unahitaji usaidizi wowote kupakua ripoti ya akaunti yako au kufuta akaunti yako, unaweza kuwasiliana nasi hapa. Kando na hayo, sera yetu inayohusiana na watumiaji wasiotumia programu itatumika.