Ukurasa Mkuu wa WhatsAppUkurasa Mkuu wa WhatsAppKituo cha Msaada
WHATSAPP WEB
VIPENGELE
PAKUA
USALAMA
KITUO CHA MSAADA

Chagua lugha yako

  • azərbaycan

  • Afrikaans

  • Bahasa Indonesia

  • Melayu

  • català

  • čeština

  • dansk

  • Deutsch

  • eesti

  • English

  • español

  • français

  • Gaeilge

  • hrvatski

  • italiano

  • Kiswahili

  • latviešu

  • lietuvių

  • magyar

  • Nederlands

  • norsk bokmål

  • o‘zbek

  • Filipino

  • polski

  • Português (Brasil)

  • Português (Portugal)

  • română

  • shqip

  • slovenčina

  • slovenščina

  • suomi

  • svenska

  • Tiếng Việt

  • Türkçe

  • Ελληνικά

  • български

  • қазақ тілі

  • македонски

  • русский

  • српски

  • українська

  • עברית

  • العربية

  • فارسی

  • اردو

  • বাংলা

  • हिन्दी

  • ગુજરાતી

  • ಕನ್ನಡ

  • मराठी

  • ਪੰਜਾਬੀ

  • தமிழ்

  • తెలుగు

  • മലയാളം

  • ไทย

  • 简体中文

  • 繁體中文(台灣)

  • 繁體中文(香港)

  • 日本語

  • 한국어

  • Pakua

  • Vipengele

  • Usalama

  • Kituo cha Msaada

  • Kuwa karibu

Ni jinsi gani tunaweza kukusaidia?

Unaweza kuperuzi mada hapo chini ili kupata kile unachokitafuta.
  1. Jumla
  2. Usalama na Faragha

Matumizi yasiyoidhinishwa ya ujumbe wa kiotomatiki au mwingi kwenye WhatsApp

WhatsApp ni jukwaa la kutuma ujumbe kwa faragha lililobuniwa ili kuwasaidia watu kuwasiliana na marafiki na wapendwa wao. Baada ya muda tumeona jinsi watu wanavyothamini kuwasiliana kwa ujumbe na biashara na kwa hivyo tumeunda zana mbili, programu ya WhatsApp Business na Jukwaa la WhatsApp Business, ili kuzisaidia kampuni kudhibiti mtagusano na wateja. Bidhaa zetu hazikusudiwi kutuma ujumbe mwingi au kiotomatiki, vyote ambavyo kwa kawaida vimekuwa ukiukaji wa Masharti yetu ya Huduma.

Tumejitolea kudumisha asili ya faragha ya jukwaa na kuhakikisha usalama wa watumiaji wasipatwe na unyanyasaji. Hivi majuzi tulifafanua uwezo wa jukwaa letu kutambua na kupiga akaunti marufuku katika waraka huu rasmi. Tunafahamu kuwa baadhi ya kampuni hujaribu kukwepa mifumo yetu ya mashine kujifunza, hata tunapojitahidi kuiboresha. Kwa kutumia taarifa za kiwango cha jukwaa zinazopatikana kwenye WhatsApp tumegundua na kuzuia mamilioni ya akaunti za unyanyasaji zisitumie huduma yetu.

Hii ni changamoto ambayo inahitaji mbinu kamili na WhatsApp imejitolea kutumia rasilimali zilizopo ikiwa ni pamoja na hatua za kisheria kuzuia unyanyasaji unaokiuka Masharti yetu ya Huduma, kama vile utumaji ujumbe wa kiotomatiki au mwingi au matumizi yasiyo ya binafsi. Hii ndiyo sababu pamoja na utekelezaji wa teknolojia, tunachukua pia hatua za kisheria dhidi ya watu binafsi au kampuni ambazo tuna ushahidi wa kwenye jukwaa kuhusu unyanyasaji kama huo. WhatsApp ina haki ya kuendelea kuchukua hatua za kisheria katika hali kama hizo.

Zaidi ya hivyo, kuanzia tarehe 7 Desemba, 2019, WhatsApp itachukua hatua za kisheria dhidi ya wale tunaoamua kuwa wanahusika na au wanawasaidia wengine katika unyanyasaji unaokiuka Masharti yetu ya Huduma, kama vile kutuma ujumbe wa kiotomatiki au mwingi au matumizi yasiyo ya binafsi, hata kama uamuzi huo umetokana na taarifa ambazo zinapatikana nje ya jukwaa letu pekee. Kwa mfano, taarifa za nje ya jukwaa zinajumuisha madai ya umma kuhusu uwezo wa kampuni kutumia WhatsApp kwa njia zinazokiuka Masharti yetu. Hii ni ilani kwamba tutachukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni ambazo tuna ushahidi wa nje ya jukwaa kuhusu unyanyasaji, ikiwa unyanyasaji huo utaendelea baada ya tarehe 7 Desemba, 2019 au ikiwa kampuni hizo zinahusishwa na ushahidi wa unyanyansaji ulio kwenye jukwaa letu kabla ya tarehe hiyo.

Hakuna chochote katika tangazo hili kinapunguza haki ya WhatsApp kutekeleza Masharti yake ya kutumia teknolojia, kama vile kupiga marufuku akaunti kwa kutegemea uainishaji unaotokana na mashine kujifunza, WhatsApp itaendelea kufanya hivyo.

Tutaendelea kutoa uwezo wa kusaidia biashara kuwasiliana na wateja wao. Kw maelezo zaidi kuhusu uwezo kama huo, tembelea Programu ya WhatsApp Business na kurasa za Jukwaa la WhatsApp Business.

Makala haya yamekusaidia?
NdiyoLa
Kwanini makala hii haikukufaidi?
  • Makala hii ilikuwa na mkanganyiko
  • Makala hii haikujibu swali langu
  • Suluhisho si sahihi
  • Sipendi kipengele au sera
Asante kwa maoni yako
Kituo cha Msaada

WHATSAPP

Vipengele

Usalama

Pakua

WhatsApp Web

Biashara

Faragha

KAMPUNI

Kuhusu

Kazi

Kituo cha Bidhaa

Kuwa karibu

Blog

Hadithi za WhatsApp

PAKUA

Mac/PC

Android

iPhone

MSAADA

Kituo cha Msaada

Twitter

Facebook

Virusi vya Korona

2022 © WhatsApp LLC

Faragha na Masharti