Ukurasa Mkuu wa WhatsAppUkurasa Mkuu wa WhatsAppKituo cha Msaada
WHATSAPP WEB
VIPENGELE
PAKUA
USALAMA
KITUO CHA MSAADA

Chagua lugha yako

  • azərbaycan

  • Afrikaans

  • Bahasa Indonesia

  • Melayu

  • català

  • čeština

  • dansk

  • Deutsch

  • eesti

  • English

  • español

  • français

  • Gaeilge

  • hrvatski

  • italiano

  • Kiswahili

  • latviešu

  • lietuvių

  • magyar

  • Nederlands

  • norsk bokmål

  • o‘zbek

  • Filipino

  • polski

  • Português (Brasil)

  • Português (Portugal)

  • română

  • shqip

  • slovenčina

  • slovenščina

  • suomi

  • svenska

  • Tiếng Việt

  • Türkçe

  • Ελληνικά

  • български

  • қазақ тілі

  • македонски

  • русский

  • српски

  • українська

  • עברית

  • العربية

  • فارسی

  • اردو

  • বাংলা

  • हिन्दी

  • ગુજરાતી

  • ಕನ್ನಡ

  • मराठी

  • ਪੰਜਾਬੀ

  • தமிழ்

  • తెలుగు

  • മലയാളം

  • ไทย

  • 简体中文

  • 繁體中文(台灣)

  • 繁體中文(香港)

  • 日本語

  • 한국어

  • Pakua

  • Vipengele

  • Usalama

  • Kituo cha Msaada

  • Kuwa karibu

Ni jinsi gani tunaweza kukusaidia?

Unaweza kuperuzi mada hapo chini ili kupata kile unachokitafuta.
  1. Jumla
  2. Usalama na Faragha

Jinsi ya kuwa salama kwenye WhatsApp

Usalama na ulinzi wako na wa ujumbe wako ni muhimu kwetu. Tunataka ujue kuhusu zana na vipengele ambavyo tumeunda ili kukusaidia kuwa salama unapotumia WhatsApp.

Masharti Yetu ya Huduma

Njia moja tunayokusudia kuwa salama kwenye WhatsApp ni kupitia Masharti yetu ya Huduma. Masharti yetu ya Huduma yanabainisha shughuli zilizopigwa marufuku, ambazo ni pamoja na kushiriki maudhui (kwenye hali, picha ya jalada au ujumbe) ambayo ni kinyume cha sheria, ya aibu, ya kukashifu, ya kutisha, ya kunyanyasa, ya chuki, ya kukera na ya kikabila au yanayochochea au kuhimiza mwenendo ambao ni kinyume cha sheria au vinginevyo hayafai au yanakiuka Masharti yetu ya Huduma. Tutampiga marufuku mtumiaji ikiwa tutaamini kwamba mtumiaji huyo anakiuka Masharti yetu ya Huduma.

Kwa taarifa zaidi kuhusu au mifano ya shughuli ambazo zinakiuka Masharti yetu ya Huduma, tafadhali kagua sehemu ya "Matumizi Yanayokubalika ya Huduma Zetu" kwenye Masharti yetu ya Huduma. Unaweza pia kupata maelezo zaidi kuhusu kupiga akaunti marufuku hapa.

Uwe makini na unachoshiriki

Tunakuhimiza ufikirie kwa makini kabla ya kuamua kushiriki kitu na unaowasiliana nao kwenye WhatsApp. Tafakari kama ungependa wengine waone kile ulichotuma.

Unaposhiriki soga, picha, video, faili au ujumbe wa sauti na mtu mwingine kwenye WhatsApp, atakuwa na nakala ya ujumbe huu. Atakuwa na uwezo wa kusambaza au kushiriki ujumbe huu na wengine akiamua kufanya hivyo. Kwa maelezo zaidi kuhusu kutazama mara moja, soma makala haya.

Pia WhatsApp ina kipengele cha mahali ambacho unaweza kukitumia kushiriki mahali pako kwenye ujumbe wa WhatsApp. Unapaswa tu kushiriki mahali pako na watu unaowaamini pekee.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia WhatsApp kwa uwajibikaji kwenye makala haya.

Vipengele vya usalama na ulinzi

Kwenye WhatsApp, tumetengeneza udhibiti fulani wa msingi ambao unaweza kuurekebisha kama inavyofaa kukusaidia kuwa salama.

Mipangilio ya faragha

Rekebisha mipangilio yako ya faragha ili kudhibiti ni nani anayeweza kuona taarifa zako. Unaweza kuweka mara yako ya mwisho kuonwa, picha ya jalada au hali katika mojawapo ya zifuatazo:

  • Kila mtu: Mara yako ya mwisho kuonwa, picha ya jalada au hali zitapatikana kwa watumiaji wote wa WhatsApp.
  • Waasiliani wangu: Mara yako ya mwisho kuonwa, picha ya jalada au hali zitapatikana kwa waasiliani walio kwenye kitabu chako cha anwani pekee.
  • Hakuna mtu: Mara yako ya mwisho kuonwa, picha ya jalada au hali hazitaonekana kwa mtu yeyote.

Pata maelezo kuhusu mipangilio hii ya faragha: Android | iPhone

Taarifa za kusomwa

Unaweza pia kuzima taarifa za kusomwa. Ukizima taarifa za kusomwa, hutaweza kutuma au kupokea taarifa za kusomwa. Kumbuka taarifa za kusomwa hutumwa wakati wote kwa soga za kikundi, hata kama umezima chaguo hilo kwenye mipangilio ya faragha yako. Pata maelezo zaidi kuhusu taarifa za kusomwa kwenye Android, iPhone, au KaiOS.

Pata maelezo kuhusu mipangilio hii ya faragha kwenye: Android | iPhone

Kuzuia au kuripoti waasiliani na ujumbe

Tunakuhimiza uripoti maudhui na waasiliani wanaotatiza kwetu. Unaweza kudhibiti ni nani unatangamana naye kwa kuzuia anwani mahususi au kuripoti ujumbe au anwani kwenye WhatsApp. Unapopokea picha au video za kutazama mara moja, unaweza kuripoti akaunti hiyo papo hapo kwetu kwa kutumia sehemu ya kuangalilia maudhui. Fahamu kinachotokea unapotumia vipengele vya kuzuia na kuripoti na jinsi ya kufanya hivyo, kwenye makala haya.

Rasilimali za ziada za usalama

Ikiwa unahisi wewe au mtu mwingine yeyote yuko hatarini, tafadhali wasiliana na huduma za dharura za eneo lako.

Ikiwa unaamini kuwa mtu fulani anataka kujiumiza na unajali usalama wake, tafadhali wasiliana na huduma za dharura za mahali ulipo au nambari ya simu ya kuzuia kujitoa uhai.

Ukipokea au kukutana na maudhui yanayoonyesha kwamba mtoto ananyanyaswa au kudhulumiwa, tafadhali wasiliana na Kituo cha Taifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC). Unaweza pia kuripoti mtumiaji huyo. Pata maelezo zaidi kuhusu kuripoti hapa. Tafadhali usiweke picha yoyote ya skrini ya maudhui hayo kwenye ripoti yako.

Rasilimali zinazohusiana

Jinsi ya kutumia WhatsApp kwa kuwajibika

Makala haya yamekusaidia?
NdiyoLa
Kwanini makala hii haikukufaidi?
  • Makala hii ilikuwa na mkanganyiko
  • Makala hii haikujibu swali langu
  • Suluhisho si sahihi
  • Sipendi kipengele au sera
Asante kwa maoni yako
Kituo cha Msaada

WHATSAPP

Vipengele

Usalama

Pakua

WhatsApp Web

Biashara

Faragha

KAMPUNI

Kuhusu

Kazi

Kituo cha Bidhaa

Kuwa karibu

Blog

Hadithi za WhatsApp

PAKUA

Mac/PC

Android

iPhone

MSAADA

Kituo cha Msaada

Twitter

Facebook

Virusi vya Korona

2022 © WhatsApp LLC

Faragha na Masharti