Wakati mwingine, unaweza kuona ujumbe huo hapo juu badala ya uliotumwa kutoka kwa mwasiliani. Kutokana na ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, huenda ukahitaji kusubiri ujumbe wa mtu fulani ufike kwa sababu simu yao inahitaji kuwa mtandaoni ili kukufumbulia ujumbe kwa usahihi. Hii inaweza kutokea kwa kawaida ikiwa wewe au mtu unayepiga soga naye alisakinisha upya WhatsApp hivi karibuni.
Kuharakisha mchakato huu, unaweza kujaribu kumuuliza mtu unayemtumia ujumbe afungue WhatsApp kwenye simu yao.
Kwa taarifa zaidi kuhusu ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, tafadhali soma waraka wetu rasmi na makala haya.