Arifa ya Badiliko la Msimbo wa Usalama
Soga zilizofumbwa mwisho hadi mwisho kati yako na mtu mwingine huwa zina msimbo wa usalama unaotumiwa kuthibitisha kuwa simu na ujumbe unaotuma kwenye soga hiyo umefumbwa mwisho hadi mwisho. Msimbo huu unapatikana kwenye skrini ya maelezo ya mwasiliani, kama msimbo wa QR pamoja na nambari ya tarakimu-60. Misimbo hii ni ya kipekee kwa kila soga na zinaweza kulinganishwa kati ya watu katika kila soga ili kuthibitisha kwamba ujumbe unaotuma kwenye soga umefumbwa mwisho hadi mwisho. Misimbo ya usalama ni matoleo ya wazi yenye ufunguo maalum unaoshirikihwa kati yako - na usiwe na wasiwasi, sio ufunguo halisi, hiyo huwekwa kwa siri.
Wakati mwingine, misimbo ya usalama inayotumiwa kwenye ufumbaji wa mwisho hadi mwisho inaweza kubadilika. Hili linaweza kutokea kwa sababu wewe au mwasiliani wako amesakinisha upya WhatsApp au amebadilisha simu.
Kupokea arifa wakati misimbo ya usalama imebadilika:
- Fungua WhatsApp Mipangilio.
- Gusa Akaunti > Usalama.
- Kutoka hapa, unaweza kuwezesha arifa za usalama kwa kugusa Onyesha Arifa za Usalama.
Kumbuka: Kipengele hiki kinapatikana tu ikiwa unawasiliana na mtu katika soga iliyofumbwa mwisho hadi mwisho.
Unaweza kuthibitisha kuwa msimbo wa usalama wa mwasiliani wako ni halali. Pata maelezo ya jinsi ya kufanya hivyo kwenye makala haya kuhusu ufumbaji wa mwisho hadi mwisho.