Kituo cha Msaada
Chagua lugha yako
  • azərbaycan
  • Afrikaans
  • Bahasa Indonesia
  • Melayu
  • català
  • čeština
  • dansk
  • Deutsch
  • eesti
  • English
  • español
  • français
  • Gaeilge
  • hrvatski
  • italiano
  • Kiswahili
  • latviešu
  • lietuvių
  • magyar
  • Nederlands
  • norsk bokmål
  • o‘zbek
  • Filipino
  • polski
  • Português (Brasil)
  • Português (Portugal)
  • română
  • shqip
  • slovenčina
  • slovenščina
  • suomi
  • svenska
  • Tiếng Việt
  • Türkçe
  • Ελληνικά
  • български
  • қазақ тілі
  • македонски
  • русский
  • српски
  • українська
  • עברית
  • العربية
  • فارسی
  • اردو
  • বাংলা
  • हिन्दी
  • ગુજરાતી
  • ಕನ್ನಡ
  • मराठी
  • ਪੰਜਾਬੀ
  • தமிழ்
  • తెలుగు
  • മലയാളം
  • ไทย
  • 简体中文
  • 繁體中文
  • 日本語
  • 한국어
  • WhatsApp Web
  • Vipengele
  • Pakua
  • Usalama
  • Kituo cha Msaada
  • Pakua
  • Vipengele
  • Usalama
  • Kituo cha Msaada
  • Kuwa karibu

Ni jinsi gani tunaweza kukusaidia?

Unaweza kuperuzi mada hapo chini ili kupata kile unachokitafuta.
JumlaUsalama na Faragha

Kuwalinda watumiaji wetu dhidi ya shambulizi la kupigiwa simu ya video mtandaoni

Mwezi Mei mwaka 2019 tulisimamisha shambulizi changamano la mtandaoni ambalo lilitumia mfumo wetu wa kupiga simu za video ili kutuma programu hasidi kwenye vifaa vya mkononi vya baadhi ya watumiaji wetu wa WhatsApp. Shambulizi hilo halikuwahitaji watumiaji walio lengwa kujibu simu waliyopigiwa. Tuliongeza ulinzi mpya kwa haraka kwenye mifumo yetu na kutoa sasisho kwenye WhatsApp ili kudumisha usalama wa watu wetu. Sasa tunachukua hatua za ziada, kutokana na yale ambayo tumejifunza kufikia sasa.

Tulituma ujumbe maalum wa WhatsApp moja kwa moja kwa takribani watumiaji 1,400 ambao tunaamini waliathiriwa na shambulizi hili ili kuwafahamisha kuhusu kilichotokea. Wajuzi wa usalama mtandaoni kwa jina The Citizen Lab, ambao ni kikundi cha watafiti wa kiakademia walio katika Kitivo cha Munk, Chuo Kikuu cha Toronto, walijitolea kutusaidia kuelewa zaidi kuhusu athari ya shambulizi hili kwa mashirika ya kijamii, wakiwemo wanahabari na watetezi wa haki za binadamu. The Citizen Lab imechapisha taarifa kuhusu shambulizi hili hapa na ipo tayari kutoa usaidizi kwa jumuiya hii.

WhatsApp inajali zaidi kuhusu faragha na usalama wa watumiaji wetu. Baadhi ya matukio ya binafsi zaidi katika maisha yako hushirikishwa kupitia WhatsApp, ndiyo maana tumebuni ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwenye programu yetu. Shambulizi hili liliundwa ili kufikia ujumbe baada ya kufumbilwa kwenye kifaa kilichoathiriwa, hivyo kutumia mianya kwenye programu na mifumo ya uendeshaji inayotumika kwenye simu zetu.

Tunakubaliana na mwito wa Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa wa Uhuru wa Kujieleza David Kaye kuhusu kusitishwa kwa mashambulizi haya. Sharti kuwa na uangalizi thabiti wa kisheria juu ya silaha za kimtandao kama iliyotumika kwenye shambulizi hili ili kuhakikisha kuwa hazitumiwi kukandamiza haki za watu binafsi na uhuru wao wa kujieleza popote walipo duniani. Makundi ya haki za binadamu yamenakili mtindo wa kusikitisha wa jinsi zana kama hizo zimetumiwa kuwashambulia wanahabari na watetezi wa haki za binadamu. Kwa kushirikiana na wataalamu wa utafiti waliopo the Citizen Lab, tunaamini kwamba shambulizi hili liliwalenga angalau washiriki 100 wa mashirika ya kijamii, hii ni ishara dhahiri ya kudhulumu. Idadi hii inaweza kuongezeka kadri waathiriwa wengi wanavyojitokeza. Tumejitolea kufanya kila tuwezalo, tunashirikiana na wadau katika tasnia ili kuwalinda watumiaji wetu dhidi ya aina hizi za vitisho.

WhatsApp pia imewasilisha malalamiko katika mahakama ya Marekani na inadai kwamba shambulizi lilitokana na kampuni ya vidadisi inayoitwa NSO Group pamoja na kampuni yake mama, Q Cyber Technologies. Lalamiko linadai kwamba kampuni hiyo ilikiuka sheria za Marekani na California pamoja na Masharti ya Huduma ya WhatsApp WhatsApp, zinazopiga marufuku aina hii ya utumiaji mbaya. Hii ndiyo mara ya kwanza ambapo mtoa huduma za utumaji ujumbe uliofumbwa anachukua hatua za kisheria dhidi ya shirika binafsi ambalo limeshambulia watumiaji wake. Katika malalamiko yetu tunafafanua jinsi NSO ilifanya shambulizi hili, ikiwemo ungamo kutoka kwa mfanyakazi wa NSO kwamba juhudi zetu za kukabili shambulizi zilifaa. Tunaomba katazo la kudumu la NSO kupigwa marufuku isitumie huduma zetu.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu maoni yetu yaliyochapishwa hapa.

Ikiwa ulipokea ujumbe kutoka kwetu na una maswali ya ziada kuhusu tukio hili, unaweza kutuma ujumbe moja kwa moja na kwa njia salama kwa timu ya WhatsApp kwa kufungua WhatsApp Mipangilio > Msaada > Wasiliana Nasi.

Makala haya yamekusaidia?
NdiyoLa
Kwanini makala hii haikukufaidi?
  • Makala hii ilikuwa na mkanganyiko
  • Makala hii haikujibu swali langu
  • Suluhisho si sahihi
  • Sipendi kipengele au sera
Asante kwa maoni yako
Kituo cha Msaada

WhatsApp

  • Vipengele
  • Usalama
  • Pakua
  • WhatsApp Web
  • Biashara
  • Faragha

Shirika

  • Kuhusu
  • Kazi
  • Kituo cha Bidhaa
  • Kuwa karibu
  • Blog
  • Hadithi za WhatsApp

Pakua

  • Mac/PC
  • Android
  • iPhone

Msaada

  • Kituo cha Msaada
  • Twitter
  • Facebook
  • Virusi vya Korona
2021 © WhatsApp LLC
Faragha na Masharti