Jinsi ya kubadilisha mipangilio yako ya faragha
Kimsingi, WhatsApp huweka mipangilio yako ya faragha kurusuhu:
- Mtumiaji yeyote kuona mara ya mwisho ulipokuwa mtandaoni, picha ya jalada, taarifa kuhusu na taarifa za kusomwa
- Walio kwenye anwani yako waone masasisho yako ya hali
- Mtumiaji yeyote kukuongeza kwenye vikundi
Kubadilisha mipangilio ya faragha
- Kwenye:
- Android: Gusa Chaguo zaidi
> Mipangilio > Akaunti > Faragha. - iPhone: Gusa Mipangilio > Akaunti > Faragha.
- KaiOS: Bofya Chaguo > Mipangilio > Akaunti > Faragha.
- Kompyuta ya mezani: Gusa Menyu
> Mipangilio > Faragha.
- Android: Gusa Chaguo zaidi
Unaweza kubadilisha anayeweza:
- Kuona mara yako ya Mwisho Kuonwa
- Kuona Picha yako ya Jalada
- Kuona taarifa Kukuhusu
- Kuona masasisho yako ya Hali
- Kuona Taarifa za Kusomwa
- Kukuongeza kwenye Vikundi
Kumbuka:
- Ikiwa hushirikishi mara yako ya mwisho kuonwa, hutaweza kuona mara ya mwisho watumiaji wengine walipokuwa mtandaoni.
- Ukizima taarifa za kusomwa, hutaweza kuona taarifa za kusomwa kutoka kwa watumiaji wengine. Taarifa za kusomwa hutumwa kwa soga za vikundi kila mara.
- Ikiwa mtu aliye kwenye anwani zako amezima taarifa za kusomwa, hutaweza kuona ikiwa ameona sasisho lako la hali.
- Hakuna njia ya kubadilisha nani anaweza kuona kama upo mtandaoni au unaandika....