Jinsi ya kubadilisha mipangilio ya faragha ya kikundi
Kwenye Android, iPhone na KaiOS, unaweza kuamua ni nani anaweza kukuongeza kwenye kikundi kwa kurekebisha Mipangilio yako ya WhatsApp.
Kumbuka: Mabadiliko kwenye mipangilio ya faragha ya kikundi hayawezi kufanywa kwenye WhatsApp Web au Desktop, lakini mipangilio kwenye simu yako itasawazishwa na WhatsApp Web na WhatsApp Desktop.
Kila mtu: Kila mtu, wakiwemo wasio kwenye kitabu cha anwani cha simu yako, wanaweza kukuongeza kwenye vikundi bila idhini yako.
Waasiliani Wangu: Waasiliani tu walio kwenye kitabu chako cha anwani, wanaweza kukuongeza kwenye vikundi bila idhini yako. Ikiwa mtawala wa kikundi ambaye hayupo kwenye kitabu chako cha anwani akijaribu kukuongeza kwenye kikundi, atapata ibukizi itakayomwambia hawezi kukuongeza na itamuuliza aguse Alika kwenye Kikundi au bonyeza Endelea, ikifuatwa na kitufe cha kutuma, kutuma mwaliko wa kikundi binafsi kupitia soga ya kibinafsi. Utakuwa na siku tatu za kukubali mwaliko kabla ya muda wake kuisha.
Waasiliani Wangu Isipokuwa...: Waasiliani tu walio kwenye kitabu chako cha anwani, isipokuwa wale unaowatenga, wanaweza kukuongeza kwenye vikundi bila idhini yako. Baada ya kuchagua Waasiliani Wangu Isipokuwa... unaweza kutafuta au kuchagua waasiliani wa kutowajumuisha. Msimamizi wa kikundi ambaye hujamjumuisha akijaribu kukuongeza kwenye kikundi, atapata arifa itakayomwambia hawezi kukuongeza na itamuuliza aguse Alika kwenye Kikundi ikifuatiwa na kitufe cha tuma, ili akutumie mwaliko wa kujiunga na kikundi kupitia soga ya binafsi. Utakuwa na siku tatu za kukubali mwaliko kabla ya muda wake kuisha.