Huenda umepokea barua taka kutoka kwa mtu mwingine asiyeidhinishwa na sio WhatsApp.
Tunafanya kazi kwa bidii kupunguza jumbe zozote za barua taka ambazo hupitia kwenye mfumo wetu. Kujenga nafasi ya usalama kwa watumiaji kuwasiliana na wengine ni kipaumbele kingine. Hata hivyo, kama zilivyo SMS au simu za kawaida, yawezekana watumiaji wengine wa WhatsApp ambao wana namba yako ya simu kuwasiliana nawe. Kwa hivyo, tungependa kukusaidia kutambua na kushughulikia jumbe hizi.
Jumbe zisizotakiwa kutoka kwa wengine wasioidhinishwa zinakuja katika njia nyingi, kama barua taka, utapeli na jumbe za uwongo. Aina hizi zote za jumbe zinafasiliwa kwa jumla kama jumbe zisizotakiwa kutoka kwa wengine wasioidhinishwa ambao hujaribu kukudanganya na kukushawishi kutenda kwa namna fulani.
Unaweza kuwa mlengwa wa mpango wa udanganyifu kama mojawapo ya yafuatayo yanaeleza kuhusu ujumbe unaopokea, kupitia WhatsApp au barua pepe:
Wakati wote tunakushauri kumzuia mtumaji, kupuuza ujumbe na kuufuta. Kujifunza zaidi kuhusu kuzuia, tafadhali soma makala hii. Kuepuka madhara kwa waasiliani wako, usisambaze jumbe hizi kwao.
Kwa habari zaidi kuhusu jumbe za utapeli kwa ujumla, tafadhali soma blogu yetu.