Maswali Yanayoulizwa Sana
Chagua lugha yako
  • azərbaycan
  • Afrikaans
  • Bahasa Indonesia
  • Melayu
  • català
  • čeština
  • dansk
  • Deutsch
  • eesti
  • English
  • español
  • français
  • Gaeilge
  • hrvatski
  • italiano
  • Kiswahili
  • latviešu
  • lietuvių
  • magyar
  • Nederlands
  • norsk bokmål
  • o‘zbek
  • Filipino
  • polski
  • Português (Brasil)
  • Português (Portugal)
  • română
  • shqip
  • slovenčina
  • slovenščina
  • suomi
  • svenska
  • Tiếng Việt
  • Türkçe
  • Ελληνικά
  • български
  • қазақ тілі
  • македонски
  • русский
  • српски
  • українська
  • עברית
  • العربية
  • فارسی
  • اردو
  • বাংলা
  • हिन्दी
  • ગુજરાતી
  • ಕನ್ನಡ
  • मराठी
  • ਪੰਜਾਬੀ
  • தமிழ்
  • తెలుగు
  • മലയാളം
  • ไทย
  • 简体中文
  • 繁體中文
  • 日本語
  • 한국어
  • WhatsApp Web
  • Vipengele
  • Pakua
  • Usalama
  • Maswali Yanayoulizwa Sana
  • Pakua
  • Vipengele
  • Usalama
  • Maswali Yanayoulizwa Sana
  • Kuwa karibu

Ni jinsi gani tunaweza kukusaidia?

Unaweza kuperuzi mada hapo chini ili kupata kile unachokitafuta.
JumlaUsalama na Faragha

Kuhusu ufumbaji wa mwisho hadi mwisho

Faragha na Usalama vipo kwenye damu yetu, ndiyo maana tumebuni ufumbaji wa mwisho hadi mwisho ndani ya programu yetu. Ufumbaji wa mwisho hadi mwisho ukiwepo, ujumbe wako, picha, video, ujumbe wa sauti, nyaraka, sasisho za hali na simu zinalindwa ili zisiingie kwenye mikono isiyofaa.

Utumaji Ujumbe wa Binafsi

Mfumo wa WhatsApp wa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho hutumika wakati wa soga kati yako na mtu mwingine anayetumia WhatsApp Messenger. Ufumbaji wa mwisho hadi mwisho huhakikisha kuwa ni wewe na mtu unayewasiliana naye pekee ndio mnaoweza kusoma ujumbe au kusikiliza mawasiliano na kwamba hakuna mtu yeyote katikati, hata WhatsApp yenyewe. Hii ni kwa sababu kwa kutumia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, ujumbe wenu hulindwa kwa kufuli na ni wewe na mpokeaji pekee ndio mlio na ufunguo unaohitajika kufungua na kusoma ujumbe. Haya yote hufanyika kiotomatiki: hutakiwi kuwasha mipangilio yoyote maalum ili kuhakikisha usalama wa ujumbe wako.

Utumaji Ujumbe wa Kibiashara

Kila ujumbe wa WhatsApp hulindwa na itifaki ile ile ya ufumbaji wa Signal ambao hudumisha usalama wa ujumbe kabla haujatoka kwenye kifaa chako. Unapotuma ujumbe kwenda kwenye akaunti ya biashara ya WhatsApp, ujumbe wako huwasilishwa kwa usalama kwenda sehemu iliyochaguliwa na biashara hiyo.

WhatsApp inachukulia kwamba soga kati yako na biashara zinazotumia programu ya WhatsApp Business au zinazosimamia na kujihifadhia ujumbe wa wateja huwa zimefumbwa mwisho hadi mwisho. Mara tu ujumbe ukishapokelewa, utakuwa chini ya desturi za faragha za biashara husika. Biashara hiyo inaweza kuwapa idadi fulani ya wafanyakazi, au hata mashirika mengine, jukumu la kuchakata na kujibu ujumbe.

Baadhi ya biashara1 zitaweza kuchagua kampuni kuu ya WhatsApp, ambayo ni Facebook, ili ihifadhi kwa usalama na kujibu wateja. Ingawa Facebook haitatumia ujumbe wako moja kwa moja kubaini matangazo utakayoona, biashara zitaweza kutumia soga zinazopokea kwa madhumuni yao ya kimauzo, ambayo huenda yakajumuisha kutangaza kwenye Facebook. Unaweza kuwasiliana na biashara husika wakati wowote ili upate maelezo zaidi kuhusu desturi zake za faragha.

Kumbuka: Hali ya ufumbaji wa mwisho hadi mwisho hauwezi kubadilika bila badiliko hilo kuonekana kwa mtumiaji. Kwa maelezo zaidi kuhusu ni soga zipi hufumbwa mwisho hadi mwisho, tafadhali soma waraka wetu rasmi.

Malipo

Malipo ya WhatsApp, ambayo yanapatikana kwenye nchi zilizochaguliwa, yanawezesha uhamishaji kati ya akaunti kwenye taasisi za kifedha. Kadi na namba za benki zinahifadhiwa zikiwa zimefumbwa kwenye mtandao wenye usalama sana. Hata hivyo, kwa kuwa taasisi za kifedha haziwezi kushughulikia miamala bila kupokea taarifa zinazohusiana na malipo haya, malipo haya hayakufumbwa kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho.

Skrini ya “Thibitisha Msimbo wa Usalama” kwenye maelezo ya mwasiliani ni nini?

Soga zilizofumbwa mwisho hadi mwisho huwa na msimbo wa usalama unaotumiwa kuthibitisha kuwa simu na ujumbe unazotuma kwenye soga hiyo zimefumbwa mwisho hadi mwisho.

Dokezo: Mchakato wa uthibitishaji ni wa hiari kwa soga zilizofumbwa mwisho hadi mwisho na unatumiwa tu kuthibitisha kuwa ujumbe unaotuma na simu unazopiga zimefumbwa mwisho hadi mwisho.

Msimbo huu unapatikana kwenye skrini ya maelezo ya mwasiliani, kama msimbo wa QR pamoja na nambari ya tarakimu-60. Misimbo hii ni ya kipekee kwa kila soga na zinaweza kulinganishwa kati ya watu katika kila soga ili kuthibitisha kwamba ujumbe unaotuma kwenye soga umefumbwa mwisho hadi mwisho. Misimbo ya usalama ni matoleo ya wazi yenye ufunguo maalum unaoshirikihwa kati yako - na usiwe na wasiwasi, sio ufunguo halisi, hiyo huwekwa kwa siri.

Kuthibitisha kuwa soga imefumbwa mwisho hadi mwisho:

  1. Fungua soga.
  2. Gusa jina la mwasiliani kufungua skrini ya maelezo ya mwasiliani.
  3. Gusa Ufumbaji kutazama msimbo wa QR na nambari ya tarakimu-60.
    • Kumbuka: Kipengele hiki kinapatikana tu kwa mwasiliani aliye katika soga iliyofumbwa mwisho hadi mwisho.

Ikiwa wewe na mwasiliani wako mko karibu, mmoja wenu anaweza kukagua msimbo wa QR wa mwingine au kuangalia ili kulinganisha nambari ya tarakimu-60. Ikiwa ukikagua msimbo wa QR, na msimbo huo ni sawa, alama hakikishi ya kijani itaonekana. Kwa kuwa ni sawa, unaweza kuwa na uhakika hakuna mtu anayeingilia kati ya ujumbe au simu zako.

Ikiwa misimbo haifanani, kuna uzekano kuwa unakagua msimbo wa mwasiliani tofauti, au nambari ya simu tofauti. Ikiwa mwasiliani wako amesakinisha upya WhatsApp au amebadili simu, tunapendekeza uonyeshe upya msimbo kwa kutuma ujumbe mpya na kisha kagua msimbo. Pata maelezo zaidi kuhusu mabadiliko ya misimbo ya usalama kwenye makala haya.

Ikiwa wewe na mwasiliani wako hamko karibu, waweza kumtumia nambari yenye tarakimu 60. Mjulishe mwasiliani wako kwamba mara tu apokeapo msimbo wako, anapaswa kuuandika na kisha kuulinganisha na nambari yenye tarakimu 60 inayoonekana kwenye skrini ya maelezo ya mwasiliani chini ya sehemu ya Ufumbaji. Kwa Android na iPhone, unaweza kutumia kitufe cha Shiriki kilicho katika skrini ya Thibitisha Msimbo wa Usalama ili utume nambari yenye tarakimu 60 kupitia SMS, barua pepe, nk.

Kwa nini WhatsApp inatoa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho na ina maana gani kwa kuwaweka watu salama?

Usalama ni muhimu kwa huduma ambayo WhatsApp inayotoa. Tumeona mifano mingi ambapo wadakuzi wahalifu walipata kiasi kikubwa cha data za kibinafsi kinyume na sheria na kutumia vibaya teknolojia ili kuwaumiza watu na taarifa zao zilizoibiwa. Tangu tulipomaliza utekelezaji wa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho mwaka 2016, usalama dijitali umezidi kuwa muhimu.

WhatsApp haina uwezo wa kuona maudhui ya ujumbe au kusikiliza simu zilizofumbwa mwisho hadi mwisho. Hiyo ni kwa sababu ufumbaji na ufumbuaji wa ujumbe uliotumwa na kupokelewa kwenye WhatsApp hufanyika kikamilifu kwenye kifaa chako. Kabla ya ujumbe kuondoka kwenye kifaa chako, umehifadhiwa na kufuli la ufichamishi, na mpokeaji pekee ndiye ana ufunguo. Zaidi ya hayo, funguo zinabadilika kwa kila ujumbe unaotumwa. Wakati wote haya yanatokea nyuma ya matukio, unaweza kuthibitisha kuwa mazungumzo yako yanalindwa kwa kuangalia uthibitisho wa msimbo wa usalama kwenye kifaa chako. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu utendaji huu kwenye waraka wetu rasmi.

Kwa kawaida, watu wameuliza ni nini maana ya ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwa utekelezaji wa sheria. WhatsApp inathamini kazi ambayo inafanywa na wakala za utekelezaji wa sheria kwa kuwaweka watu salama duniani kote. Kwa umakini tunahakiki, tunathibitisha na tunajibu maombi ya watekelezaji wa sheria kulingana na sheria na sera husika, na tunatoa kipaumbele kwa maombi ya dharura. Kama sehemu ya jitihada zetu za elimu, tulichapisha taarifa kwa ajili ya utekelezaji wa sheria kuhusu taarifa chache tunazokusanya na jinsi wanavyoweza kuziomba kutoka kwa WhatsApp, unaweza kuzisoma hapa.

Kujifunza kuhusu usalama wako kwenye WhatsApp, tafadhali tembelea Usalama wa WhatsApp.

1Mwaka wa 2021.

Makala hii ilikufaidi?
NdiyoLa
Kwanini makala hii haikukufaidi?
  • Makala hii ilikuwa na mkanganyiko
  • Makala hii haikujibu swali langu
  • Suluhisho si sahihi
  • Sipendi kipengele au sera
Asante kwa maoni yako
Mwanzo wa Maswali Yanayoulizwa Sana

WhatsApp

  • Vipengele
  • Usalama
  • Pakua
  • WhatsApp Web
  • Biashara
  • Faragha

Shirika

  • Kuhusu
  • Kazi
  • Kituo cha Bidhaa
  • Kuwa karibu
  • Blog
  • Hadithi za WhatsApp

Pakua

  • Mac/PC
  • Android
  • iPhone

Msaada

  • Maswali Yanayoulizwa Sana
  • Twitter
  • Facebook
  • Virusi vya Korona
2021 © WhatsApp LLC
Faragha na Masharti