Kila ujumbe wa WhatsApp hulindwa na itifaki ile ile ya ufumbaji wa Signal ambao hudumisha usalama wa ujumbe kabla haujatoka kwenye kifaa chako. Unapotuma ujumbe kwenda kwenye akaunti ya biashara ya WhatsApp, ujumbe wako huwasilishwa kwa usalama kwenda sehemu iliyochaguliwa na biashara hiyo.
WhatsApp inachukulia kwamba soga kati yako na biashara zinazotumia programu ya WhatsApp Business au zinazosimamia na kujihifadhia ujumbe wa wateja huwa zimefumbwa mwisho hadi mwisho. Mara tu ujumbe ukishapokelewa, utakuwa chini ya desturi za faragha za biashara husika. Biashara hiyo inaweza kuwapa idadi fulani ya wafanyakazi, au hata mashirika mengine, jukumu la kuchakata na kujibu ujumbe.
Baadhi ya biashara1 zitaweza kuchagua kampuni kuu ya WhatsApp, ambayo ni Facebook, ili ihifadhi kwa usalama na kujibu wateja. Ingawa Facebook haitatumia ujumbe wako moja kwa moja kubaini matangazo utakayoona, biashara zitaweza kutumia soga zinazopokea kwa madhumuni yao ya kimauzo, ambayo huenda yakajumuisha kutangaza kwenye Facebook. Unaweza kuwasiliana na biashara husika wakati wowote ili upate maelezo zaidi kuhusu desturi zake za faragha.
Kumbuka: Hali ya ufumbaji wa mwisho hadi mwisho hauwezi kubadilika bila badiliko hilo kuonekana kwa mtumiaji. Kwa taarifa kuhusu soga zipi zina ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, tafadhali soma waraka wetu rasmi.
Malipo ya WhatsApp, ambayo yanapatikana kwenye nchi zilizochaguliwa, yanawezesha uhamishaji kati ya akaunti kwenye taasisi za kifedha. Kadi na namba za benki zinahifadhiwa zikiwa zimefumbwa kwenye mtandao wenye usalama sana. Hata hivyo, kwa kuwa taasisi za kifedha haziwezi kushughulikia miamala bila kupokea taarifa zinazohusiana na malipo haya, malipo haya hayakufumbwa kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho.
WhatsApp inataka kuhakikisha kuwa unaelewa kinachofanyika kwa ujumbe wako. Ikiwa hutaki kupokea ujumbe kutoka kwa mtu au biashara, unaweza kumzuia moja kwa moja kwenye soga au umfute kutoka kwenye orodha yako ya waasiliani. Tunataka kuhakikisha kuwa unaelewa jinsi ujumbe wako unavyoshughulikiwa na kwamba una hiari unazohitaji kufanya uamuzi unaokufaa.
1Mwaka wa 2021.