Kuna ishara kadha za kuonyesha kama umezuiwa:
- Huwezi kuona tena mwisho kaonwa ya mwasiliani au akiwa mtandaoni katika dirisha la soga. Jifunze zaidi hapa.
- Huwezi kuona sasisho za picha ya jalada ya mwasiliani.
- Jumbe zozote zilizotumwa kwa mwasiliani ambaye amekuzuia utaonyesha alama ya uhakiki moja (ujumbe uliotumwa), na haiwezi kuonyesa alama ya pili ya uhakiki (ujumbe umepokelewa).
- Simu zozote unazojaribu kupiga hazitakamilika.
Ukiona ishara hizi kwa mwasiliani, hii inaweza kumaanisha kwamba mwasiliani huyo amekuzuia. Hata hivyo, kuna uwezekano mwingine. Tumefanya haya kwa makusudi kuwa na maana nyingi. ili kulinda faragha yako unapozuia mtu. Kwa hiyo, hatuwezi kukuambia kama umezuiwa na mtu mwingine.
Jifunze jinsi ya kumzuia mtu kwenye: Android | iPhone