Kuhusu kusasisha taarifa za biashara kwa akaunti za WhatsApp Business zilizounganishwa na Ukurasa wa Facebook
Unapounganisha akaunti yako ya WhatsApp Business na Ukurasa wako wa Facebook na kuwasha usawazishaji, akaunti yako ya WhatsApp Business itaonyesha taarifa za biashara zilizo kwenye Ukurasa wako wa Facebook.
Hata hivyo, tofauti na WhatsApp Business, Ukurasa wa Facebook unaweza kuwa na wahariri au wasimamizi wengi. Wasimamizi na wahariri wote wa Ukurasa wataweza kusasisha taarifa za biashara kwenye Ukurasa wako wa Facebook. Taarifa hizo zitaonekana kwenye jalada lako la WhatsApp Business.
Hata hivyo, mabadiliko yanayofanyika kwenye programu ya WhatsApp Business hayataonekana katika Ukurasa wa Facebook, hata kama akaunti zimeunganishwa.