Kuhusu taarifa za kubadilika kwa msimbo wa usalama
Soga zilizofumbwa mwisho hadi mwisho kati yako na mtu mwingine huwa zina msimbo wa usalama unaotumiwa kuthibitisha kuwa simu na ujumbe unaotuma kwenye soga hiyo umefumbwa mwisho hadi mwisho. Msimbo huu unapatikana kwenye skrini ya maelezo ya unayewasiliana naye, ukiwa msimbo wa QR pamoja na nambari yenye tarakimu 60. Misimbo hii ni ya kipekee kwa kila soga binafsi na inaweza kulinganishwa kati ya watu katika kila soga ili kuthibitisha kwamba ujumbe huo unaotuma kwenye soga umefumbwa mwisho hadi mwisho. Misimbo ya usalama ni matoleo yanayoonekana ya funguo maalum zinazoshirikiwa kati yenu - na usiwe na wasiwasi, misimbo hii si funguo halisi, funguo hizo huwa siri kila wakati.
Wakati mwingine, misimbo ya usalama inayotumiwa katika soga zilizofumbwa mwisho hadi mwisho kati yako na mtu mwingine zinaweza kubadilika. Hii inaweze kuwa ni kwa sababu wewe au mtu unayewasiliana naye amesakinisha upya WhatsApp, amebadilisha simu au ameongeza au kuondoa kifaa kilichooanishwa. Unaweza kuthibitisha kuwa msimbo wa usalama kati yako na unayewasiliana naye ni sahihi wakati wowote. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kufanya hivyo katika makala haya kuhusu ufumbaji wa mwisho hadi mwisho.
Kupokea arifa wakati misimbo ya usalama imebadilika
Unaweza kuwezesha arifa za usalama ili upokee arifa wakati msimbo wa usalama kati yako na unayewasiliana naye umebadilika kwenye soga iliyofumbwa mwisho hadi mwisho. Utahitaji kuwasha mipangilio kwenye kila kifaa ambapo unataka kupata arifa.
Kuwasha arifa za misimbo ya usalama
Android
- Fungua WhatsApp > gusa Chaguo zaidi
> Mipangilio. - Gusa Akaunti > Usalama.
- Washa Onyesha arifa za usalama kwenye simu hii.
iPhone
- Nenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp.
- Gusa Akaunti > Usalama.
- Washa Onyesha Arifa za Usalama kwenye Simu hii.
Web na Desktop
- Fungua WhatsApp > bofya Menyu
au juu ya orodha yako ya soga > Mipangilio. - Bofya Usalama.
- Washa Onyesha arifa kwenye kompyuta hii.
Kuzima arifa za msimbo wa usalama
Android
- Fungua WhatsApp > gusa Chaguo zaidi
> Mipangilio. - Gusa Akaunti > Usalama.
- Zima Onyesha arifa za usalama kwenye simu hii.
iPhone
- Nenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp.
- Gusa Akaunti > Usalama.
- Zima Onyesha Arifa za Usalama kwenye Simu Hii.
Web na Desktop
- Fungua WhatsApp > bofya Menyu
au juu ya orodha yako ya soga > Mipangilio. - Bofya Usalama.
- Zima Onyesha arifa za usalama kwenye kompyuta hii.