Jinsi ya kufuta soga ya kikundi
Unaweza kufuta kikundi kutoka kwenye simu yako ikiwa wewe ni mtawala wa kikundi na uondoe kila mshiriki. Baada ya kuondoa washiriki wote, utahitaji kutoka kwenye kikundi ili uone hiari ya kufuta kikundi.
Ondoa mshiriki
- Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa au bofya mada ya kikundi.
- Gusa au bofya mshiriki unayetaka kuondoa. Kisha:
- Kwa Android: Gusa Ondoa {mshiriki} > SAWA.
- Kwa iPhone: Gusa Ondoa kwenye Kikundi > Ondoa.
- Kwa Web/Desktop: Bofya Menyu
kwa jina la mshiriki > Ondoa > ONDOA.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kutoka na kufuta vikundi: Android | iPhone | WhatsApp Web na Desktop