Jinsi ya kuunda vibandiko vya WhatsApp
Tumetoa sampuli za programu na msimbo wa Android na iOS, ili kurahisisha kuweka mchoro wa kibandiko chako na kuunda programu inayohitaji tu uzoefu mdogo wa kuendeleza au kuandika programu. Waendelezaji wa juu wanaweza pia kuunda programu za kibandiko ya hali ya juu kutumia seti ya API na kiolesura ambazo WhatsApp inawezesha.
Soma mahitaji hapa chini ya kuunda vibandiko vyako mwenyewe na tazama mafaili ya NISOME yanayohusiana na sampuli za programu kwa orodha kamili ya mahitaji na vidokezo unavyohitaji kuunda programu yako ya kibandiko.
Kumbuka: Ili kuzingatia Miongozo ya Duka la Programu la Apple wakati wa kuunda programu ya kibandiko cha iOS, hakikisha kuendeleza kiolesura ya kipekee ya mtumiaji (UI) na usitumie UI za sampuli za programu zetu.
Vibandiko vya kawaida lazima vikidhi mahitaji yafuatayo:
- Kila kibandiko kiwe na mandharinyuma ya wazi.
- Vibandiko lazima viwe na pikseli 512x512 kamili.
- Kila kibandiko lazima iwe chini ya KB 100.
Lazima pia utoe ikoni ambayo itatumiwa kuwakilisha kifurushi chako cha kibandiko kwenye kichagua au trei ya kibandiko cha WhatsApp. Picha hii iwe na pikseli 96x96 na lazima iwe chini ya KB 50.
Pamoja na mahitaji ya hapo juu, tunashauri sana zifuatazo:
- Vibandiko vitatafsiriwa kwenye mandhari mbalimbali, ikiwa ni pamoja na nyeupe, nyeusi, rangi na muundo. Tunapendekeza uongeze mstari wa pikseli-8 #FFFFFF nje ya kila kibandiko. Tazama sampuli ya faili la Photoshop (PSD) hapa.
- Inapaswa kuwa na pembe ya pikseli-16 kati ya picha ya kibandiko na upande wa turuba ya pikseli ya 512x512.
Ikiwa una maswali au masuala unapounda vibandiko, tafadhali tutumie barua pepe kwa developers@support.whatsapp.com. Kwa maswali au masuala mengine, wasiliana nasi kwa WhatsApp kwa kuenda kwa Mipangilio > Msaada > Wasiliana Nasi.
Vibandiko vinapatikana kwenye toleo la hivi karibuni ya Android na iOS toleo la WhatsApp. Kama huoni vibandiko, hakikisha una sasisha kwa toleo jipya la WhatsApp kwenye duka la programu la simu yako.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kutumia vibandiko: Android | iPhone
- Kuhusu kuunda vibandiko