Jinsi ya kumzuia msimamizi wa kikundi
Kwa wakati huu, haiwezekani kuzuia kikundi. Hata hivyo, unaweza kuondoka kwenye kikundi na kumzuia msimamizi wa kikundi.
Kwenye Android, iPhone na KaiOS, unaweza kuamua nani anaweza kukuongeza kwenye vikundi kwa kubadilisha mipangilio yako ya faragha ya kikundi.
Kumzuia msimamizi ambaye nambari yake ya simu haijahifadhiwa kwenye kitabu cha anwani cha simu yako
- Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa au bofya mada ya kikundi.
- Gusa au bofya nambari ya simu ya msimamizi unayetaka kumzuia.
- Ukiulizwa, gusa au bofya Mtumie ujumbe {phone number} au Tuma Ujumbe.
- Soga tupu na msimamizi itafunguka. Gusa au bofya nambari ya simu iliyo juu.
- Gusa au bofya Zuia > Zuia.
Kumzuia msimamizi ambaye nambari yake imehifadhiwa kwenye kitabu cha anwani cha simu yako
Android
- Nenda kwenye WhatsApp > gusa Hiari zaidi
> Mipangilio > Akaunti > Faragha > Waasiliani waliozuiwa. - Gusa
. - Gusa jina la msimamizi kutoka kwenye orodha ya waasiliani.
iPhone
- Gusa WhatsApp > Mipangilio > Akaunti > Faragha > Iliyozuiwa.
- Gusa Ongeza Mpya....
- Gusa jina la msimamizi kutoka kwenye orodha ya waasiliani.
KaiOS
- Fungua WhatsApp > bonyeza Hiari > Mipangilio > SAWA.
- Chagua Akaunti > Faragha > FUNGUA.
- Chagua WALIOZUIWA > Ongeza mpya....
- Gusa jina la msimamizi kutoka kwenye orodha ya waasiliani.
- Bonyeza ZUIA.
Web na Desktop
- Bofya Menyu (
au ) juu ya orodha yako ya soga kwenye WhatsApp. - Bofya Mipangilio > Iliyozuiwa.
- Boyfa Ongeza mwasiliani aliyezuiwa.
- Tafuta kisha ubofye jina la msimamizi.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kubadilisha mipangilio ya faragha ya vikundi
- Jinsi ya kuzuia na kuruhusu waasiliani: Android | iPhone | KaiOS