Kupata orodha ya mapendeleo/waasiliani
WhatsApp inatambua kwa haraka na kwa urahisi ni nani kati ya waasiliani wako wanaotumia WhatsApp kwa kupitia kitabu cha anwani ya simu yako.
Kupata orodha ya mapendeleo/waasiliani wako nenda kwenye tab ya Soga na gusa ikoni ya Soga mpya.
Ikiwa huwaoni waasiliani wako:
- Hakikisha kuwa waasiliani wako wanatumia WhatsApp.
- Hakikisha kuwa umezihifadhi namba za simu za waasiliani wako kwenye kitabu cha anwani ya simu yako. Ikiwa wanatumia namba ya simu ya kigeni, tumia muundo wa kimataifa kamilifu.