Unaweza kusasisha WhatsApp kwa urahisi kutoka kwenye programu ya duka la simu yako. Tafadhali zingatia kwamba kama ulipokea ujumbe ambao hauwezeshwi na toleo lako la WhatsApp utahitaji kusasisha WhatsApp. Tunakuhimiza kutumia toleo la karibuni la WhatsApp. Toleo za karibuni zina vipengele vipya na suluhisho za matatizo ya programu.
Nenda kwenye Duka la Google Play na utafute WhatsApp. Gusa Sasisha karibu na WhatsApp Messenger.
Nenda kwenye Duka la Programu na utafute WhatsApp. Gusa SASISHA karibu na WhatsApp Messenger.
Bonyeza JioStore au Duka kwenye menyu ya programu. Sogeza kwa upande kuchagua Jamii, kisha chagua WhatsApp. Bonyeza SAWA au CHAGUA > SASISHA.