Android: Gusa UNGANISHA KIFAA. Fuata maelekezo kwenye skrini ikiwa kifaa chako kina uthibitishaji wa bayometriki.
iPhone: Gusa Unganisha Kifaa > Sawa. Kwenye iOS 14 na matoleo ya baadaye, tumia Touch ID au Face ID kufungua.
Chagua kisanduku tiki karibu na Nibaki nimeingia kwenye skrini ya QR katika kompyuta yako au Portal ili uwe umeingia katika akaunti kwenye kifaa hiki.
Tumia simu yako kuchanganua msimbo wa QR ulio kwenye kompyuta au Portal yako.
Ukiulizwa, gusa au chagua Nimemaliza.
Kumbuka: Uthibitishaji hushughulikiwa na mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako kwa kutumia alama za bayometriki zilizohifadhiwa humo. WhatsApp haiwezi kufikia taarifa za bayometriki zilizohifadhiwa kwenye mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako.
Kuondoka
Unaweza kuondoka kwenye WhatsApp Web au WhatsApp Desktop kutokea kwenye simu yako, kompyuta au kifaa cha Portal.
Kuondoka kwenye kompyuta au Portal yako
Fungua WhatsApp Web au WhatsApp Desktop.
Bofya Menyu ( au ) juu ya orodha ya soga zako > Ondoka.