Kuhusu kutoka kwenye WhatsApp Messenger kwenda kwenye WhatsApp Business
WhatsApp Business ni programu unayoweza kupakua bila kulipia, iliyoundwa kwa kuwazingatia wamiliki wa biashara ndogo. Ina vipengele vinavyozingatia biashara kama vile jalada la biashara na ujumbe wa kiotomatiki vinavyorahisisha kutangamana na wateja na kutangaza biashara yako. Pia, inahisi na kufanya kazi kama WhatsApp Messenger.
Kwa biashara ambazo kwa sasa zinatumia WhatsApp Messenger, kuhamia WhatsApp Business kunachukua hatua chache tu. Baada ya kuthibitisha nambari yako kwenye WhatsApp Business, unaweza kuchagua maudhui yako yote (k.m., vibandiko unavyopendelea, mandhari), mapendeleo ya soga (k.m., soga zisizo na arifa, milio ya soga), na historia ya soga itolewe kwenye WhatsApp Messenger na kuhamishiwa kwenye WhatsApp Business.
Kumbuka: Kuhamisha taarifa zako zote kutoka kwenye WhatsApp Business kurudi kwenye WhatsApp Messenger bado hakufanyi kazi kwa wakati huu. Ukichagua kurudi kwenye WhatsApp Messenger, utapoteza vipengele vya biashara pamoja na soga na maudhui yaliyoundwa ulipokuwa unatumia WhatsApp Business.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kuhama kutoka kwenye WhatsApp Messenger kwenda kwenye WhatsApp Business: Android | iPhone
- Kuhusu programu ya WhatsApp Business