Maelezo ya mwasiliani hayaonekani
Mipangilio ya faragha inakuruhusu kuficha mara ya mwisho kuonwa kwako, picha ya jalada, kuhusu, hali, au taarifa za kusomwa. Unaweza usione maelezo ya mtu mwingine kwa sababu ya vile walivyoweka mipangilio yao ya faragha.
Ikiwa huoni mara ya mwisho kuonwa ya mtu mwingine, picha ya jalada, kuhusu, hali, au taarifa za kusomwa za mtu mwingine, inaweza kuwa kwa sababu moja ya yafuatayo:
- Mwasiliani wako amebadilisha mipangilio yake ya faragha kuwa Hakuna mtu.
- Umebadilisha mipangilio yako ya faragha ya mwisho kaonwa kuwa Hakuna mtu.
- Mwasiliani wako amebadilisha mipangilio yao ya faragha kuwa Waasiliani Wangu , na haujahifadhiwa kama mwasiliani kwenye simu yao.
- Umezuiwa na mwasiliani.
- Kunaweza kuwa na tatizo la muunganisho.
- Mwasiliani wako hajaweka picha ya jalada.