Jinsi ya kuangalia duka la Facebook kwenye WhatsApp
Kumbuka: Huenda bado usiweze kutumia kipengele hiki.
WhatsApp inaruhusu biashara kuunganisha akaunti zao za WhatsApp Business na duka la Facebook, hivyo kuwarahisishia wateja kukagua bidhaa na huduma zilizo katika duka bila kuondoka kwenye WhatsApp.
Biashara ambazo zimeunganisha akaunti zao na duka la Facebook huwa na aikoni ya mfuko wa kununulia unaoonekana karibu na jina la biashara kwenye soga.
Kukagua duka la Facebook kwenye WhatsApp
- Fungua soga kati yako na biashara ambayo ungependa kukagua duka lake.
- Gusa aikoni ya mfuko wa kununulia karibu na jina la biashara.
- Duka la biashara hiyo kwenye Facebook litafunguka kwenye WhatsApp. Kutoka hapa, tumia upau wa kutafutia kutafuta vitu mahususi au telezesha kidole kwenye duka ili uchunguze bidhaa na huduma zote ambazo biashara inatoa.