Jinsi ya kutuma ujumbe kwa biashara kwenye WhatsApp kutoka kwenye Duka lao la Facebook
Kumbuka: Huenda bado usiweze kutumia kipengele hiki.
Unapotembelea Duka la Facebook la biashara, unaweza kutumia kitufe cha Ujumbe kuanzisha mazungumzo na biashara kuhusu bidhaa unayoangalia.
Tuma ujumbe wa WhatsApp Business kutoka kwa Duka lao la Facebook
- Kutoka kwa ukurasa wa bidhaa kwenye duka, gusa Ujumbe. WhatsApp itafungua na kuanzisha soga na akaunti ya WhatsApp Business ya duka.
- Ili kukusaidia kuanzisha mazungumzo, kiolezo cha ujumbe kitaonekana kwenye uga wa matini. Kiolezo hiki kinaweza kuhaririwa kusema chochote utakachopenda. Kiungo chako kwa ukurasa wa bidhaa uliokuwa ukitazama kwenye duka kitaambatanishwa pia kwenye ujumbe wako.
- Gusa
au .
Ili uone ukurasa wa bidhaa au duka moja kwa moja kwenye WhatsApp, gusa kiungo kilichoambatishwa kwenye ujumbe uliotumia biashara. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kushiriki na kuangalia viungo vya kurasa za bidhaa za duka kwenye WhatsApp katika makala haya.
Kumbuka: Hatua hizi zina husu tu kwa Maduka ambayo yamechagua WhatsApp kama njia yao ya msingi ya mawasiliano.