WhatsApp inaruhusu kuumba maandishi kwenye jumbe zako. Tafadhali zingatia, hamna hiari ya kuzima kipengele hiki.
Kuweka italiki kwenye ujumbe wako, weka mstari pande zote mbili za maandishi:
_maandishi_
Kuweka herufi nzito kwenye ujumbe wako, weka nyota pande zote mbili wa maandishi:
*maandishi*
Kuweka mkato ulalo kwenye ujumbe wako, weka kiwimbi pande zote mbili za maandishi:
~maandishi~
Kuweka nafasi moja kwenye ujumbe wako, weka alama tatu za kunukuu pande zote mbili za maandishi:
```maandishi```
Kumbuka:
Mbadala, unaweza kutumia njia mkato kwenye Android na iPhone.
Android: Gusa na shikilia maandishi unayo ingiza kwenye sehemu ya maandishi, kisha chagua Herufi nzito *, *Italiki *, au *Zaidi
iPhone: Gusa maandishi unayo ingiza kwenye sehemu ya maandishi > Chagua au Chagua Yote > B_I_U. Kisha, chagua Herufi nzito, Italiki, Mkato ulalo, au Nafasi moja.