Kuhusu "mwisho kaonwa" na "mtandaoni"
Mwisho kaonwa na mtandaoni hukuambia muda wa mwisho ambapo watu unaowasiliana nao walitumia WhatsApp, au ikiwa wapo mtandaoni.
Ukiona mtu unayewasiliana naye yupo mtandaoni, basi amefungua WhatsApp kwenye kifaa chake na ameunganishwa kwenye intaneti. Hata hivyo, haimaanishi kuwa mtumiaji amesoma ujumbe wako.
Mwisho kaonwa hurejelea muda wa mwisho ambapo mtu unayewasiliana naye alitumia WhatsApp. Kupitia mipangilio yetu ya faragha, una chaguo la kudhibiti nani anaweza kuona mara ya mwisho ulipoonekana. Huenda usiweze kuona hali ya kuwa mtandaoni kwa mtu isipokuwa kama amekuhifadhi katika anwani zake au alikutumia ujumbe hapo awali. Tafadhali kumbuka huwezi kudhibiti ni nani anaweza kuona hali yako ya kuwa mtandaoni katika mipangilio.
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kufanya usione maelezo ya mwisho kuonwa kwa mtu unayewasiliana naye:
- Anaweza kuwa ameweka mipangilio yake ya faragha ili kuficha maelezo haya.
- Inawezekana umeweka mipangilio yako ya faragha ili usishirikishe mwisho wa kuonwa. Ikiwa hushirikishi mwisho wa kuonwa kwako, hutaweza kuona mwisho wa kuonwa kwa watu wengine unaowasiliana nao.
- Unaweza kuwa umezuiwa.