Kuhusu nakala iliyofumbwa mwisho hadi mwisho
Ufumbaji wa mwisho hadi mwisho huhakikisha kuwa ni wewe na mtu unayewasiliana naye pekee ndio mnaoweza kusoma ujumbe au kusikiliza mawasiliano na kwamba hakuna mtu yeyote katikati, hata WhatsApp yenyewe. Kupitia nakala iliyofumbwa mwisho hadi mwisho, unaweza pia kuongeza safu ile ile ya ulinzi kwa nakala yako ya soga kwenye iCloud au Hifadhi ya Google.
Ulinzi wa nenosiri
Unapounda nakala rudufu iliyofumbwa mwisho hadi mwisho, ujumbe na maudhui yako huhifadhiwa kwenye iCloud na kulindwa kwa nenosiri au ufunguo wenye tarakimu 64. Unaweza kubadilisha nenosiri lako wakati wowote ilimradi unaweza kufikia nenosiri la awali au ufunguo.
Kumbuka: Hutaweza kurejesha nakala yako ikiwa utapoteza soga zako za WhatsApp na usahau nenosiri au ufunguo wako. WhatsApp haiwezi kuweka upya nenosiri lako au kurejesha nakala kwa niaba yako.
Kuzima uwekaji wa nakala iliyofumbwa mwisho hadi mwisho
Unaweza kuchagua kuzima nakala rudufu iliyofumbwa mwisho hadi mwisho kwa kutumia nenosiri lako au ufunguo au kwa kuthibitisha kwa bayometriki zako au PIN ya kifaa. Ukizima uwekaji wa nakala liliyofumbwa mwisho hadi mwisho, ujumbe na maudhui yako hayatahifadhiwa tena kwenye huduma za wingu isipokuwa kama ukipangilia kufanya hivyo.
Uwekaji nakala katika kifaa cha iPhone
Ikiwa umewasha uwekaji nakala rudufu kwenye iCloud kwa ajili ya kila kitu kwenye iPhone yako, pia nakala ya historia ya soga zako isiyofumbwa itahifadhiwa kwenye iCloud. Ili kuhakikisha kwamba soga zako za WhatsApp na maudhui yamenakiliwa kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho pekee, zima Nakala Rudufu ya iCloud kwenye kifaa chako.
Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyokusanya na kuchakata data yako, pamoja na nakala rudufu iliyofumbwa mwishi hadi mwisho, tafadhali angalia Sera za Faragha za WhatsApp.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kuwasha na kuzima uwekaji wa nakala iliyofumbwa mwisho hadi mwisho
- Sikumbuki nenosiri la nakala iliyofumbwa