Unaweza kutuma ujumbe unaotoweka kwenye WhatsApp kwa kuwezesha ujumbe unaotoweka. Baada ya kuwezeshwa, ujumbe mpya unaotumwa kwenye soga ya binafsi au ya kikundi utatoweka baada ya siku saba. Uteuzi wa hivi karibuni unadhibiti ujumbe wote kwenye soga. Mpangilio huu hautaathiri ujumbe wa awali ulioutumwa au kupokelewa kwenye soga. Kwenye soga ya kibinafsi, mtumiaji yeyote anaweza kuwasha au kuzima ujumbe unaotoweka. Kwenye soga ya kikundi, wasimamizi wa kikundi tu ndiyo wanaweza kuwasha au kuzima ujumbe unaotoweka.
Kumbuka: Tumia ujumbe unaotoweka na watu wanaoaminika tu. Kwa mfano, inawezekana kwa mtu fulani:
Kwa kawaida, midia unayopokea kwenye WhatsApp itapakuliwa kiotomatiki kwenye picha zako. Kama umewasha hali ya ujumbe unaotoweka, midia inayotumwa kwenye soga itatoweka, lakini itahifadhiwa kwenye simu kama umewasha hali ya kupakua kiotomatiki. Unaweza kuzima hali ya kupakua kiotomatiki kwenye WhatsApp Mipangilio > Hifadhi na Data.