Ni rahisi kutofautisha kati ya akaunti ya kibinafsi na akaunti ya biashara kwenye WhatsApp. Kwenye soga, gusa jina la mwasiliani ili kuona jalada lake. Ikiwa ni biashara, jalada lake litakuwa na mojawapo ya lebo zifuatazo:
- Akaunti rasmi ya biashara: WhatsApp imeamua kuwa chapa inayojulikana na halisi inamiliki akaunti hii. "Akaunti rasmi ya biashara" ina beji ya alama hakikishi ya kijani kwenye jalada lake na kando ya kichwa kwenye mtungo wa soga. Jina la biashara hiyo linaonekana hata ikiwa haujaongeza biashara hiyo kwenye kitabu chako cha anwani.
- Akaunti ya biashara: Hii ni hali ya chaguo-msingi kwa biashara ambayo inaunda akaunti kwenye mojawapo ya bidhaa za WhatsApp Business.
Dokezo: "Akaunti rasmi ya biashara" haionyeshi kuwa WhatsApp inaidhinisha biashara hii.
Rasilimali zinazohusiana