Imeshindwa kuunganisha kwenye WhatsApp
Ikiwa huwezi kuunganisha kwenye WhatsApp, kwa kawaida ni kwa sababu kifaa chako hakijaunganishwa kwenye intaneti. Ili kuhakikisha una muunganisho wa intaneti unaofanya kazi, fuata hatua zifuatazo:
- Hakikisha una kifurushi cha data ya mtandao wa mtoa huduma unayetumia mtandao wake, au una muunganisho wa Wi-Fi ulio na intaneti.
- Hakikisha kuwa nguvu ya ishara ya mtandao wa Wi-Fi au data ya simu ni nzuri na kwamba kifaa chako kimeunganishwa kwenye mtandao.
- Fungua ukurasa wa tovuti kwenye kivinjari chako ili uone kama inafunguka. Ikiwa unafunguka, basi kifaa chako kimeunganishwa kwenye intaneti.
- Washa upya kifaa chako.
Ikiwa bado huwezi kuunganisha
Ikiwa huwezi kuingia kwenye intaneti kupitia mtandao wa data wa simu yako, jaribu mtandao mmoja au zaidi wa Wi-Fi. Iwapo unaweza kufungua kurasa za tovuti na kuendesha programu nyingine kwenye intaneti, lakini WhatsApp haiunganishwi, unaweza kujaribu kutatua matatizo yako ya muunganisho kwenye: Android | iPhone
Ikiwa unaweza kuunganisha programu nyingine kupitia mtandao wako wa data, lakini WhatsApp haijaweza, huenda ni kwa sababu anayekupa huduma za data ameweka mipangilio ili kuzuia programu fulani za soga. Jaribu hili ikiwa WhatsApp bado haifanyi kazi kwenye data tu:
- Wasiliana na watoaji wako wa data ya simu za mkononi na umuulize kuhusu mipangilio tofauti ya ufikiaji wa kufungua programu za soga.
- Atakuongoza kwenye mchakato ambao utaweka mipangilio ya mtandao wako wa data na mipangilio ya tovuti.
Rasilimali zinazohusiana:
Imeshindwa kuunganisha kwenye WhatsApp kwenye Android | iPhone | KaiOS | Web au Desktop