Usishirikishe msimbo wako wa uthibitisho wa SMS ya WhatsApp na wengine, hata kama ni marafiki au familia. Ikiwa umeshawishiwa kushirikisha msimbo wako na kupoteza ufikiaji wa akaunti yako ya WhatsApp, soma maagizo hapa chini ili urejeshe akaunti yako.
Ikiwa unashuku kuwa mtu mwingine anatumia akaunti yako ya WhatsApp, unapaswa kuwajulisha familia na marafiki kwani mtu huyu anaweza kukuiga kujifanya ni wewe katika soga na vikundi. Tafadhali kumbuka, WhatsApp imefumbwa mwisho hadi mwisho na ujumbe umehifadhiwa kwenye kifaa chako, kwa hivyo mtu anaye fikia akaunti yako kwenye kifaa kingine hawezi kusoma mazungumzo ya zamani.
Ingia kwenye WhatsApp na nambari yako ya simu na thibitisha nambari yako ya simu kwa kuingiza msimbo wa tarakimu-6 uliyopokea kupitia SMS. Jifunze zaidi kuhusu kuthibitisha nambari yako ya simu kwenye Kituo chetu cha Msaada: Android | iPhone.
Mara uingizapo msimbo wa tarakimu 6 wa SMS, mtu anayetumia akaunti yako atatolewa nje kiotomatiki.
Unaweza kuulizwa kutoa msimbo wa uhakiki wa hatua mbili. Kama hujui msimbo huu, mtu anayetumia akaunti yako anaweza kuwa amewezesha msimbo wa uhakiki wa hatua-mbili. Ni lazima usubiri siku 7 kabla ya kuingia bila msimbo wa uhakiki wa hatua mbili. Bila kujali kama unajua msimbo huu wa kuthibitisha, yule mtu mwingine ametolewa kwenye akaunt mara tu ulipoingiza msimbo wa tarakimu 6 wa SMS. Jifunze zaidi kuhusu uhakiki wa hatua mbili kwenye makala haya.